Tundu Lissu amjibu Spika Ndugai.
Utaratibu wa matibabu ya mbunge umewekwa na sheria ya Bunge iitwayo Sheria ya Uendeshaji wa Bunge ya 2008. Kifungu cha 24(1) cha Sheria hiyo kinasema "matibabu ya mbunge yatagharamiwa na Bunge ndani na nje ya Tanzania."
Kwa utaratibu wa sasa ulivyo, Bunge linalipia gharama za tiba na gharama za kujikimu za mbunge na ndugu anayemuuguza.
Sheria ya Uendeshaji wa Bunge haijaweka masharti anayoyazungumzia Spika Ndugai. Hakuna kifungu chochote kinachozungumzia kibali cha Muhimbili au cha Magufuli.
Ukweli ni kwamba kauli ya Spika Ndugai inathibitisha jinsi ambavyo Bunge limepoteza mamlaka na hadhi yake chini ya uongozi wake dhaifu. Hata masuala ambayo Sheria haijampa Rais mamlaka, Spika Ndugai ameyakabidhi kwa Magufuli.
Kauli hiyo ni uthibitisho pia wa jinsi ambavyo Bunge linaendeshwa bila kufuata sheria, kwa chuki na upendeleo wa kisiasa chini ya uongozi wa Spika Ndugai.
Yeye amekwenda India mara nyingi kutibiwa kabla na baada ya kuwa Spika kwa gharama za Bunge. Mimi mbaya wao niliyepigwa risasi nikiwa nahudhuria vikao vya Bunge ninakataliwa matibabu kwa sababu zisizokuwa na msingi wowote.
Tatu, wala sio kweli kwamba sikufuata utaratibu, kama maana ya neno hilo ni utaratibu uliowekwa na sheria.
Katika mazingira ya jaribio la mauaji dhidi yangu, utaratibu pekee uliokuwa unawezekana ulikuwa ni kunihamisha nchini kwa dharura.
Nilikuwa nimeumizwa vibaya, mifupa imevunjwa kila mahali, nimepoteza damu nyingi na risasi zimejaa tumboni.
Kusema nisubiri kibali cha Bunge au cha Muhimbili au cha Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi. Pengine ndicho Spika Ndugai na wakubwa wake walichokitaka. Mungu aliwakatalia, sasa wamenuna.
Na hivi ni kweli sikupata kibali cha kupelekwa Nairobi???
Uamuzi wa kunipeleka Nairobi ulifanywa kwenye kikao kilichofanyika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Spika Ndugai na Naibu wake walikuwepo kwenye kikao hicho. Katibu wa Bunge wakati, Dr. Tom Kashililah, alikuwepo. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wake Dr. Ulisubisya Mpoki walikuwepo. Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba alikuwepo. Na Mwenyekiti Mbowe na wabunge kadhaa walihudhuria pia.
Baada ya kukubaliana kwamba napelekwa Nairobi, ndege ililetwa Dodoma saa sita za usiku. Uwanja wa Ndege wa Dodoma hauruhusu ndege kuruka au kutua baada ya saa 12 jioni. Nani aliyeruhusu ndege iliyonichukua kutua na kuruka saa sita usiku kama hakukuwa na kibali cha Bunge???
Lakini waovu waliotaka kuniua wanazidi kujidhihirisha. Nilipigwa risasi masaa mawili baada ya Magufuli kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kulinda rasilimali za nchi hata kama vitavunja sheria za nchi yetu.
Mazingira ya tukio yanadhihirisha njama za mauaji yaliyopangwa au kuelekezwa kutoka juu: ulinzi wote uliondolewa mahali ninapoishi; na barabara za maeneo yote ya jirani zilifungwa.
Baada ya tukio CCTV ya kwenye jengo ninamokaa iliondolewa na Jeshi la Polisi kimya kimya na haijawahi kutolewa maelezo yoyote.
Hakuna uchunguzi wala upelelezi wowote uliofanywa na polisi. Hata kidanganyio cha kuja kunihoji mimi na dereva wangu Nairobi kiliwashinda. Wanajua mpango mzima.
Sasa, baada ya dana dana nyingi, Spika Ndugai anasema sijatibiwa na Bunge kwa sababu sikupata kibali cha Jiwe Magufuli!!! Of course Jiwe hawezi kutoa kibali hicho. Alitaka niuawe, atatoaje kibali cha kunitibu?!?!?!
Kuhusu kupatiwa matibabu na Serikali ya Ujerumani, huu ni uongo usiokuwa tofauti na wa yule mtu anayeitwa Musiba.
Spika Ndugai ametoa kauli hii kwa sababu ukweli ni kwamba hajui na hajawahi kujua natibiwaje. Angeuliza angepewa taarifa sahihi, lakini hajawahi kuuliza.
Ukweli ni huu. Gharama zote za tiba zinagharamiwa na bima ya afya ya Ubelgiji ambayo mimi na mke wangu tulijiunga mara baada ya kufika hapa.
Gharama za bima, ambazo kwa hapa sio kubwa sana, nimelipia mwenyewe.
Gharama za kujikimu kama kupanga nyumba, chakula, usafiri, n.k. ni michango ya Wasamaria Wema Watanzania na wasio Watanzania. Ni wengi sana na wengi wao sijawahi hata kuwaona au kuwafahamu.
Hawa ndio wameniwezesha mimi na mke wangu kuishi hapa Ubelgiji kwa miezi yote ambayo tumekuwa hapa na sijawahi kuacha kuwatambua na kuwashukuru kwa wema na upendo wao.
Hii habari ya tiba ya Wajerumani ni mwendelezo wa propaganda dhaifu kwamba CHADEMA inatumiwa na Wajerumani. Ni ujinga mtupu.
Tundu Lissu.

0 Comments:
Post a Comment