Mwili wa Mtanzania, Leyla Mtumwa anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe, Kema Kasambula, mwezi uliopita jijini London nchini Uingereza umewasili nchini usiku huu.
Mwili huo umepokelewa usiku huu Jumatatu, Aprili 23, 2018 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupelekwa nyumbani kwao. Kaloleni Arusha kwa ajili ya shughuli za maziko yanayotarajiwa kufanyika kesho kwa babu yake maeneo ya Sinoni.


0 Comments:
Post a Comment