Aliyekuwa 'Video Queen' Agnes Gerald maarufu 'Masogange' amefariki dunia, leo Ijumaa katika Hospitali ya kwa Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Wakili wake, Reuben Simwanza amethibitisha hilo pamoja na wasanii mbalimbali nyota ambao wameweka picha zake kuonesha masikitiko yao akiwemo mwigizaji Steve Nyerere na wengineo.
Hivi karibuni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5, baada ya kupatikana na kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya heroin na Oxazepam.
Wasanii mbalimbali kupitia kurasa zao za Instagram na Twitter wameonesha kushtushwa kwao na taarifa hizo na kumuombea apumzike kwa amani.
Mungu ailaze Roho yake Mahali pema peponi
Source Azam

0 Comments:
Post a Comment