Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dk. Vincent Mashinji amesema sharti la kuripoti kituo Kikuu cha Kati cha Polisi ni gumu kulingana na kazi wanazozifanya.
Ameyasema hayo leo baada ya yeye na Viongozi wenzake wa chama hicho kuripoti kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya sharti la dhamana walilopewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Dr. Mashinji amesema, “Iliamuriwa na mahakama kila siku ya Ijumaa turipoti kwa RPC hapa Central Polisi ikiwa kama sehemu ya sharti la dhamana tulilopewa mahakamani kwenye ile kesi yetu inayojumuisha watu 9”
“Kimsingi ukiangalia ni sharti gumu kwani 'nature' ya kazi zetu inatutaka kusafiri kwenda kujenga chama, hivyo tunashindwa ila kwa vile ni amri ya mahakama lazima tutekeleze kwani ndio inatenda haki,” -Dr. Mashinji.

0 Comments:
Post a Comment