Watoto 32, walimu wawili na dereva waliokufa kwenye ajali.
Aliyasema hayo jana wakati akiahirisha shauri hilo linalovuta hisia za wengi baada ya kukwama kuendelea kutokana na wakili wa serikali, Alice Mtenga kuiomba mahakama impe muda wa kufanyia marekebisho hati ya mshitaka.
Shauri hilo lilikuwa limekuja mahakamani hapo kwa upande wa jamhuri kuendelea kuleta mashahidi wake ambapo jana alitarajiwa kufika shahidi wa nne ambaye ijumaa alifika lakini hakuweza kutoa ushahidi wake kutokana na wakili wa utetezi Method Kimomogoro kutokuwepo mahakamani hapo.
Wakili wa Serikali, Mtenga aliiomba mahakama ipange siku nyingine kwa ajili ya kufanyia marekbisho hati ya mashitaka aliyodai kuwa inamapungufu na haitawezekana shauri hilo kuendalea kabla ya kufanyiwa marekebisho.
Kwa upande wake wakili wa utetezi, Kimomogoro alisema hana pingamizi na ombi hilo isipokuwa akataka marekebisho hayo yafanyike haraka ili shauri hilo liendelee leo kwani lilikuwa limepangiwa kusikilizwa siku tatu mfululizo.
“Kama nilivyosema kesi hii tulipanga isikilizwa siku tatu hivyo kikitokea cha kukwamisha tutasikiliza ndani ya hizohizo siku tatu, nilikuwa nikimaanisha kuwa kesi iishe ndani ya wiki hii, kwa upande wa mashitaka basi tuatendelea kesho (leo) na kama kitatokea cha kutukwamisha basi nitachukua hatua manake sikatazwi kuifuta,” alisema hakimu Kamugisha wakati akiharisha shauri hilo.
Awali akiahirisha shauri hilo ijumaa iliyopita hakimu Kamugisha alipanga lisikilizwe siku tatu mfulilizo kuanzia jana mpaka lifikie mwisho kwani limekaa muda mrefu mahakamani.
Alimuagiza wakili wa Serikali, Mtenga kuwaandaa mashahidi wake ili watoe ushahidi wao siku hiyo ambapo wakiweza kumaliza siku ya kwanza siku inayofuata upande wa utetezi wataendelea endapo wataonekana wana kesi ya kujibu.
"Hii ni ya muda mrefu na haikupaswa kuchukua muda mrefu hivyo. Mimi ' spirit' yangu ni hii kesi iishe nitaipangia siku ya kusikiliza mashahidi wote na siku nyingine ya kusikiliza upande wa utetezi kama watakuwa na kesi ya kujibu nataka mpaka mwezi ujao uamuzi uwe umetolewa na ninapopanga tarehe sitaki ' excuse' yoyote," alisema hakimu Kamugisha na kuongeza.
"Naipangia siku nzima ya tarehe saba tusipomaliza tutaendelea tarehe nane isipoisha tutaendelea tarehe tisa mpaka hili shauri lifike mwisho tusiendelee kulichelewesha kwa sababu haki i liyocheleweshwa ni haki iliyopita,".
Shauri hilo limekuwa likiahirishwa mfululizo tokea mwezi novemba mwaka jana kutokana na hakimu Kamugisha kutuwa mahakamani hapo kutokana na majukumu mengine ya kikazi.
Tayari mashahidi watatu wameshafika mbele ya mahakama hiyo akiwemo, Mkuu wa Usalama barabarani mkoani Arusha, Nuru Seleman, (43), koplo Hamad na Afisa wa Idara ya Kazi mkoani Arusha, Wilfred Mdumi, (38).
Awali katika kesi hiyo ambayo mmiliki wa shule ya Lucky Vicent, Innocent Moshi anakabiliwa na mashitaka manne huku mwalimu Mkuu msaidizi Longino Nkana, (38) akikabiliwa na shitaka moja.
Shauri hilo namba 78/2017 linalovuta hisia za wengi jijini hapa wanadaiwa kuruhusu abiria 13 waliozidi kuingia kwenye gari kinyume na utaratibu na sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo vya wanafunzi 32,walimu wawili na dereva mmoja .
Nuda alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa wa kwanza anadaiwa mnamo Mei 6, mwaka huu eneo la kwa Morombo akiwa mmiliki wa gari aina ya Mitsubishi Rosa, lenye namba za usajili T 871 BYS, aliruhusu gari hilo kufanya biashara ya kubeba abiria likiwa halina leseni.
Alisema katika shitaka la pili Moshi anadaiwa kuruhusu gari hilo kuendeshwa bila kuwa na bima na shitaka la tatu ni kushindwa kuwa na mkataba na dereva wake ambaye kwa sasa ni marehemu,Dismas Gasper.
Mmiliki huyo wa Lucky Vicent alisomewa shitaka la nne analodaiwa kuruhusu gari lake kubeba abiria waliozidi uwezo wa gari ambapo abiria 13 walizidi.
Mnamo Mei 6, mwaka huu wanafunzi 32 ,walimu wawili na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent waliofariki kwa ajali eneo la Rhotya ,wakielekea mjini Karatu katika shule ya msingi Tumaini kufanya mtihani wa ujirani mwema.

0 Comments:
Post a Comment