VIDEO MBUNGE WA CHADEMA ATUNUKIWA TUZO INDIA


MBUNGE wa Viti maalum Chadema, amepewa tuzo ya heshima kwa harakati anazoendesha kusaidia wanawake na watoto nchini.


Mwakagenda ambaye ni Mwanaharakati wa siku nyingi wa Wanawake na Watoto alipewa   tuzo hiyo inayotambulika kama "A Woman of the decade in Public life".

 Mbunge huyo anayewakilisha mkoa wa Mbeya alipewa jana tuzo hiyo kwenye Mkutano maalumu wa jukwaa la wanawake la Uchumi linalofanyikia New Delh nchini India.

Mkutano huo ulioanza April 26, mwaka huu na unatarajiwa kumalizika leo  ambapo umewashirikisha Wanawake zaidi ya 2000 kutoka pande mbalimbali za dunia wakiwemo Viongozi na wale walioonyesha mabadiliko chanya katika jamii.


Katika mkutano huo Mwakagenda pia alipata fursa ya kuongea na Wanawake hao kutoka pande zote za dunia na pia amekuwa mwanamke pekee kwa Afrika Mashariki kukabidhiwa tuzo hiyo.



 Mwakagenda ametunukiwa tuzo hiyo  kutokana na mchango wake mkubwa wa muda mrefu katika kusaidia wanawake na watoto nchini Tanzania ikiwemo kielimu, kiafya na kiuchumi ikiwemo juhudi zake anazofanya katika kuwawezesha wanawake katika msaada wa kisheria na katika kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwasaidia vifaa vya kufanyia shughuli zao ikiwemo vyerehani na vifaa vingine.

0 Comments:

Post a Comment