Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana Jumanne, Desemba 15, 2020 ameshuhudia uingizwaji majini wa Kivuko cha MV Kilindoni ‘Hapa kazi Tu’ kitakachofanya safari zake kati ya Nyamisati na Mafia, tukio hilo limefanyika Karakana ya Kujenga na Kukarabati vivuko ya Songoro iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam.
Katika hotuba yake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango na kuwanufaisha watumiaji.
Waziri Mkuu amesema kuwa ujenzi wa kivuko hicho unatokana na Utashi wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kwamba ahadi zote zilizowekwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) zinatekelezwa ili Watanzania waweze kuthibitisha kuwa CCM inaahidi na kutekeleza.


0 Comments:
Post a Comment