AFCON 2027: CPA Makalla Ataka Waliolipwa Fidia Kupisha Mradi wa Bilioni 87.9 Arusha

 



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, ametoa agizo zito kwa wananchi wote waliolipwa fidia kupisha ujenzi wa miundombinu ya barabara za kujiandaa na Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027). 

Agizo hilo linalenga kumpa nafasi mkandarasi kuendelea na kazi hiyo bila vikwazo.


Makalla alitoa agizo hilo kufuatia ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi na upanuzi wa miundombinu hiyo yenye urefu wa kilometa 9.1. Mradi huu mkubwa unatekelezwa kwa njia nne na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 87.9.

Maeneo Yanayohusika na Upanuzi wa Barabara
Mradi huo unajumuisha maeneo muhimu yafuatayo jijini Arusha:

  • Makutano ya Ngarenaro – Mzunguko wa Kisongo
  • Makutano ya Ngarenaro – Kona ya Nairobi

  • Makutano ya Ngarenaro – Soko la Kilombero
  • Kauli ya RC CPA Amos Makalla
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Makalla alimshukuru Rais kwa kutoa fedha hizo na kuwasihi wadau wote kushirikiana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

"Nimshukuru  Rais kwa kuwezesha ujenzi wa barabara hizi, niwaombe watalamu wa sekta zote kutoa ushirikiano kuhakikisha hakuna kizuizi kwa Mkandarasi kufanya kazi. Serikali ishawalipa fidia wananchi wote kwa barabara zote za AFCON. Zaidi ninawashukuru ambao wameshaondoka, wameonesha uzalendo, na ambao hawajaondoka niwaombe waondoke ili kupisha ujenzi."

Manufaa Makubwa ya Mradi Huu Jijini Arusha
Kukamilika kwa miundombinu hii kutaleta mapinduzi makubwa kiuchumi na kijamii katika Jiji la Arusha:
Kuchochea Utalii na AFCON 2027: Barabara hizi zitakuwa kiungo muhimu wakati wa michuano na zitaboresha sekta ya utalii.
  1. Kupunguza Msongamano: Zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya foleni za magari jijini Arusha.
  2. Kutokomeza Mafuriko: Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Massawe, amebainisha kuwa mradi huu utajenga mitaro mikubwa ya kupeleka maji Mto TANAPA. Hii itaondoa kabisa kero ya mafuriko katika maeneo ya Majengo, Shamsi, na Ngarenaro.
Ujenzi huu ni hatua kubwa kuelekea maandalizi ya AFCON 2027 na maboresho ya kudumu ya Jiji la Arusha.

0 Comments:

Post a Comment