Waswahili husema nyumba njema haikosi wageni na hii imedhihirika leo tarehe 4 Agosti, 2026 baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mhe Zubeir Ali Maulid kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Aidha, haitoshi Spika Zubeir alielezwa kuhusiana na maajabu ya mchanga unaohama uliopo eneo la Olduvai ambapo mamia ya watu ambao mapenzi yao yamelega lega humiminika katika eneo hilo kuimarisha mapenzi.
Kwa mujibu wa simulizi za kihistoria kutokana na mchanga huo kuwa na asili ya sumaku wapendao wakifika mahali hapo penzi huwa motomoto na kuimarika.
Akizungumza baada ya ziara hiyo Spika Zubeir ametoa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii ili kujifunza na kupata utulivu.
Spika Zubeir ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kulinda uhifadhi, kusimamia utalii na maendeleo ya jamii.




0 Comments:
Post a Comment