SHINYANGA: Zaidi ya abiria 40 waliokuwa wakisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Kagera wamenusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Abood walilokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto.
Ajali hiyo imetokea leo, Ijumaa Novemba 13, 2026, majira ya saa 11:00 alfajiri katika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Basi lililohusika katika ajali hiyo lina namba za usajili T 285 EAV.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, SSP Stanley Luhwago, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa kikosi chake kilifika eneo la tukio kwa wakati na kufanikiwa kuudhibiti moto huo bila kuleta madhara kwa binadamu.
"Abiria wote zaidi ya 40 waliokuwamo ndani ya basi hilo wamefanikiwa kutoka salama na hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa," imeeleza taarifa ya mamlaka za uokoaji.
Hadi sasa, chanzo cha moto huo pamoja na thamani halisi ya mali iliyoteketea bado havijajulikana, huku vyombo husika vikiendelea na uchunguzi wa kina kubaini chanzo chake.
Habari za Tanzania, Ajali ya Moto, Basi la Abood, Kahama, Shinyanga, Jeshi la Zimamoto
0 Comments:
Post a Comment