Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dkt.Abdul-Razaq Badru, amewataka waongoza watalii nchini kuendelea kujiongezea maarifa kuhusu vivutio na bidhaa za utalii ili kuboresha huduma kwa wageni.



Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Waongoza Watalii wa Kanda ya Kaskazini (NTSGS) Dkt.Badru alisema mtu anayetafuta maarifa hachoki hasa ikizingatiwa kuwa waongoza watalii ni kiungo muhimu kati ya vivutio vya utalii na wageni hivyo wanapaswa kuwa na uelewa wa kina wa maeneo wanayoyaeleza. 



Alisema mtalii anayefika nchini anatarajia kupata taarifa sahihi na za kutosha kuhusu vivutio anavyotembelea, jambo ambalo huongeza thamani ya huduma anayolipia na kumhamasisha kurejea tena nchini. 


Dkt.Badru aliongeza kuwa utalii ni miongoni mwa sekta zinazochangia kwa kiwango kikubwa uchumi wa taifa, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote, wakiwemo waongoza watalii, katika kuendeleza sekta hiyo. 


Amewahakikishia waongoza watalii kuwa Ngorongoro kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kuandaa mafunzo ya kujengea uwezo, ikiwemo mafunzo maalum ya kuwaboresha kitaaluma kabla ya msimu mkubwa wa utalii na tukio kubwa na la muhimu kabisa la Michezo ya AFCON. 



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NTSGS, Angelbert Aloyce Qorro, alisema chama hicho tangu kuanzishwa mwaka 2019 kimekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha taaluma ya uongozaji watalii na kujenga ushirikiano na taasisi za uhifadhi.

  


▪️Ni Leseni za Uchimbaji wa Kati(ML) na Leseni za Utafiti(PL)


▪️Ni maeneo ambayo wananchi waliwasilisha malalamiko kwenye ziara ya Waziri Mkuu


▪️Waziri Mavunde aelekeza vikundi vya wachimbaji wadogo kupewa Leseni kwenye maeneo hayo


▪️Ni utekekelezaji wa maelekezo ya Mh Rais Samia juu ya wachimbaji wadogo kupewa maeneo


▪️Wananchi wa Katavi waishukuru Serikali kwa hatu hii


Katavi



Waziri wa Madini Anthony ameelekeza kufutwa kwa  leseni kubwa saba ikiwemo Leseni ya Uchimbaji wa Kati (ML) na Leseni za Utafiti (PL) mkoani Katavi.


Maelekezo hayo, yametolewa leo Novemba 13, 2026 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akigawa leseni kwa vikundi tisa (9) vya wachimbaji wadogo  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Program ya (MBT), ikiwa ni mpango kufuta leseni ambazo hazifanyiwi kazi na kutolewa kwa Vijana, Wanawake na watu wenye uhitaji maalum.


Akizungumza katika hafla ya utoaji wa leseni , Waziri Mavunde amesema kuwa, utoaji wa leseni ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.


“Wakati wa ziara ya Mh. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba mliwasilisha changamoto ya upatikanaji wa maeneo ya kuchimba na Mh. Waziri Mkuu aliielekeza Wizara kuchukua hatua ili wale wote wasioendeleza maeneo yao kurejeshwa serikalini na kugawiwa kwa wachimbaji wadogo”Alisema Mavunde


Waziri Mavunde ameeleza kuwa, pamoja na wachimbaji wadogo kupatiwa fursa hiyo, pia wawekezaji wakubwa wenye nia ya kuendeleza maeneo ya uchimbaji  ndani ya katavi pia watatizamwa.


Waziri Mavunde ameeleza kuwa, mkoa wa Katavi ni mkoa wenye madini mbalimbali hivyo  lengo la serikali ni kuondoa utaratibu wa watu wachache kumiliki eneo kubwa leseni bila kuendeleza.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda , Mhe.Jamila Kimaro ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuwapatia leseni  vijana , wakina mama na watu wenye uhitaji maalum jambo litakalosaidia katika kujiendeleza na kujiunua kiuchumi.


Pia, amemshukuru Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya bilioni 296 katika wilaya ya Mpanda.


Hafla hiyo ya utoaji wa leseni , imeudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa CCM Mkoa wa Katavi na Wilaya,wataalam kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya.

 



Sumbawanga, Rukwa


Wananchi wa kijiji cha Kiyandaigonda, kata ya Kaoze Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamejawa na furaha kuelekea kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kiyandaigonda - Chombe yenye urefu wa kilomita 8.3.


Kijiji cha Kiyandaigonda ambacho ni maarufu kwa kilimo cha mpunga, mahindi, alizeti, mihogo na viazi miundombinu yake ya barabara imeharibiwa vibaya na mvua kutoka uwanda wa juu wa milima jirani na kijiji hicho ambayo imeharibu barabara na madaraja yote hivyo kusababisha changomoto ya mawasiliano ya barabara katika kijiji hicho. 


Msimamizi wa mradi huo, Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Sumbawanga Mhandisi Christopher Shija amesema, ujenzi wa barabara hiyo unaotekelezwa na TARURA kupitia mradi wa CERC umeletwa kwa malengo mahsusi kwa ajili ya kuondoa adha ambayo wananchi wa kijiji cha Kiyandaigonda ambao kwa sasa wana furaha kubwa kutokana na maendeleo mazuri ya mradi huo ambao umefikia asilimia 87 ya utekelezaji wake.


"Kulikuwa na changamoto ya upitishaji mazao na hata uhaba na gharama ya juu kwa bidhaa muhimu hasa kwa wananchi wa Kiyandaigonde, Kaoze na Chombe, kwa hatua hii ya utekelezaji iliyofikiwa baadhi ya bidhaa zimeanza kupungua bei na mazao kama mchele bei zimeanza kupungua kutokana na magari kufika mashambani kwa urahisi" amesema Mhandisi Shija.


Amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa madaraja na vivuko 18 ambapo madaraja makubwa matano na madogo ni 13 sambamba na upandishaji wa tuta la barabara lenye urefu wa km 8.3.


Ameongeza kuwa mpaka sasa jumla ya madaraja na vivuko 14 vimekamilika, vimebaki vivuko vitatu, unyanyuaji wa tuta la barabara km 8 nao umekamilika na hatua inayoendelea sasa hivi ni kuvisambaza ili kuweka changarawe kilomita zote 8.3


Kwa upande wake, Bw. Chrisant Kiliyaka Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kiyandaigonda amesema kabla ya mradi huo walikuwa na changamoto nyingi ambazo zimewadhoofisha kiuchumi. 


"Kukosa daraja na barabara ni vitu ambavyo vinaleta umaskini kwahiyo baada ya  mradi huu wananchi wamefarijika sana, ndio mana wanapambana kuja kutoa maombi ya kimila ili kufanikisha kukamilika kwa daraja na barabara ili iweze kutuletea maendeleo katika kijiji chetu" amesema Bw. Kiliyaka.


Ameongeza kuwa kiuchumi barabara hiyo ni mkombozi kwao kwani itakapokamilika itawawezesha kuuza mazao yao kwa urahisi na bei itaongezeka kwa sababu magari makubwa yataweza kufika katika kijiji chao na kusafirisha mazao.

 

SHINYANGA: Zaidi ya abiria 40 waliokuwa wakisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Kagera wamenusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Abood walilokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto.

Ajali hiyo imetokea leo, Ijumaa Novemba 13, 2026, majira ya saa 11:00 alfajiri katika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Basi lililohusika katika ajali hiyo lina namba za usajili T 285 EAV.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, SSP Stanley Luhwago, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa kikosi chake kilifika eneo la tukio kwa wakati na kufanikiwa kuudhibiti moto huo bila kuleta madhara kwa binadamu.

"Abiria wote zaidi ya 40 waliokuwamo ndani ya basi hilo wamefanikiwa kutoka salama na hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa," imeeleza taarifa ya mamlaka za uokoaji.

Hadi sasa, chanzo cha moto huo pamoja na thamani halisi ya mali iliyoteketea bado havijajulikana, huku vyombo husika vikiendelea na uchunguzi wa kina kubaini chanzo chake.


Habari za Tanzania, Ajali ya Moto, Basi la Abood, Kahama, Shinyanga, Jeshi la Zimamoto

 



Arusha, Tanzania– The East African Court of Justice (EACJ) has been urged to strengthen its role in upholding the law and ensuring compliance with regional agreements among Partner States in order to deepen regional integration, facilitate trade and attract investment across East Africa.



The call was made by Uganda’s First Deputy Prime Minister and Chairperson of the East African Community (EAC) Council of Ministers, Rebecca Alitwala Kadaga, during celebrations marking the Court’s 25th anniversary in Arusha.



Kadaga said the Court had a crucial responsibility to ensure that Partner States honour their commitments, particularly those relating to the Customs Union and Common Market, in order to eliminate barriers that hinder trade and economic cooperation.


She emphasised that a strong legal framework was fundamental to building a competitive regional market, facilitating business activities and ensuring that citizens of Partner States benefited from regional integration.



Meanwhile, EAC Secretary General Ambassador Stephen Mbundi stressed the importance of strengthening the Court’s institutional capacity to enable it to respond effectively to the growing demands of a Community expanding in membership and responsibilities.



Reflecting on the Court’s journey since its establishment, EACJ President Justice Nestor Kayobera said the increasing number of cases filed before the institution demonstrated growing confidence among citizens and Partner States in its justice delivery system.



Kayobera noted that the Court had handled various cases concerning the interpretation and application of the Treaty for the Establishment of the East African Community, including disputes involving one Partner State against another.


He said this demonstrated that Partner States continued to recognise the Court as a legal avenue for resolving disputes, rather than relying solely on dialogue.


He explained that although leaders of Partner States regularly meet to discuss common issues, certain disagreements still require judicial intervention to secure solutions in accordance with established legal procedures.


The EACJ President also urged citizens of Partner States to recognise the Court as an institution established to serve them and understand their right to access it whenever they believe that the principles of the EAC Treaty have been violated.


However, he clarified that the Court's objective was not to encourage citizens to institute proceedings against their governments, but to raise public awareness of its jurisdiction and its role in safeguarding justice and the rule of law.


Kayobera further emphasised that public confidence in the Court must go hand in hand with judicial accountability, ensuring that its decisions are grounded in the law and uphold accepted standards of justice.


In another development, he expressed appreciation to the Government of Tanzania for its continued cooperation in security and protocol matters, saying the support had enabled the Court to carry out its mandate from its headquarters in Arusha throughout its 25-year history.


He noted that, over the years, the institution had served various judges and staff members, some of whom had completed their terms of service through retirement, while others had passed away while still in office.


Speaking about the anniversary celebrations, Kayobera said the event had attracted more than 200 guests from within and outside Africa.


The participants included representatives of judicial institutions from West Africa through the Economic Community of West African States (ECOWAS), as well as delegates from South Africa, Europe and the United States.


He said the participation reflected the Court’s contribution to strengthening cooperation among judicial institutions at regional and international levels, describing the 25th anniversary as a significant milestone in the history of justice delivery within the Community.


Kayobera also clarified that the Court’s jurisdiction was limited to matters relating to the East African Community under its founding Treaty and did not extend to internal affairs of Partner States falling outside its mandate.


He added that the progress of the Community also depended on the strength of its Partner States and their institutions, stressing that each country had a responsibility to strengthen its justice systems and uphold the rule of law.


The East African Court of Justice commenced its operations on 30 November 2001 with three Partner States. The East African Community has since expanded to eight Partner States.


The Court is mandated to interpret and ensure the application of the Treaty for the Establishment of the East African Community, as well as ensure compliance with the Community’s laws.


 



KwaZulu-Natal, Afrika Kusini 11 Novemba, 2026.


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewapeleka nchini Afrika Kusini watumishi wake wanne kupata mafunzo ya wiki moja kuhusiana na Uhifadhi wa faru katika hifadhi ya Phinda  Private game Reserve  iliyopo Kwazulu Natal.



Mafunzo hayo yanatokana na ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Hifadhi ya Ngorongoro na Phinda private Game Reserve ambapo hifadhi hizi zimekuwa zikishirikiana katika kufanikisha kuwalinda wanyama hao.



Kiongozi wa Ujumbe huo, Kanali Fikiri Machibya ambaye ni mshauri wa Jeshi la Uhifadhi ameeleza kuwa mafunzo hayo yameendelea kuwasaidia kujua mbinu ambazo hifadhi ya Phinda wanazotumia kulinda, kuhifadhi,kuzuia uharibifu, kufuatilia miendendo ya wanyamapori, mimea na matumizi ya teknolojia kama njia ya kisasa na imara kwenye ulinzi katika maeneo yenye changamoto.




Afisa Mhifadhi Mwandamizi ambaye ni mratibu wa Faru Ngorongoro Deogratius Maige ameeleza kuwa; "Ili nchi au  taasisi ifanikiwe kuwahifadhi Wanyama adimu kama  Faru ni muhimu  kuwajengea uzoefu kwa vitendo  watumishi kwenye nchi  ambazo zina uzoefu mkubwa wa kuwahifadhi na kuwalinda Wanyama hao, 


Mafunzo hayo pia yamekuwa ni  sehemu ya kubadilishana uzoefu kuhusu uhifadhi shirikishi kwa jamii zinazozunguka hifadhi, wajibu wa kutoa kwa jamii (CSR), uchomaji moto maeneo ya hifadhi kuimarisha malisho, kudhibiti uvamizi wa mimea na utoaji wa ajira za muda mfupi na mrefu kwa jamii zinazosaidia shughuli za uhifadhi.


Hifadhi ya Wanyamapori Binafsi ya Phinda iliyopo Jimbo la KwaZulu-Natal Nchini Afrika kusini ina ukubwa wa hekta 29,866 na moja ya maajabu ya dunia ikijumuisha wanyama mbalimbali wakiwepo Big Five (simba, chui, tembo, faru na nyati) na zaidi ya spishi 436 za ndege na kuifanya kuwa moja ya maeneo yanayoongoza kwa wanyamapori wengi Afrika Kusini.

 



WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wanamichezo kutumia ushawishi wao kuhimiza malezi bora kwa vijana na kuwa mfano katika kulinda maadili ya jamii.



“Wanamichezo mara zote ni watu wenye kauli kubwa. Ni watu wenye sauti inayosikika. Tuendelee kuwa sauti ya malezi kwenye nchi yetu,” amesema.



Dkt. Mwigulu ametoa wito huo leo (Alhamisi, Novemba 12, 2026), akimwakilisha Makamu wa Rais,  Deogratius John Ndejembi, katika ufunguzi wa mashindano ya 56 ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.



Amesema jamii haipaswi kufumbia macho mmomonyoko wa maadili kwa kudhani kuwa unawahusu watu au familia nyingine pekee, kwani athari zake zinaweza kuenea na kulikumba Taifa.


Amewataka wanamichezo kupaza sauti kuhimiza mambo mema, kama jamii ilivyoshirikiana kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amezitaka taasisi kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu kushirikiana na mashirikisho kama SHIMMUTA ili kuwawezesha wafanyakazi kushiriki michezo mahali pa kazi.


Amesisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi mara kwa mara na kuyafanya sehemu ya maisha, badala ya kuyaona kama adhabu.


Kuhusu uendeshaji wa mashindano, Dkt. Mwigulu amewataka viongozi wa taasisi na timu kuhakikisha wanawasilisha majina ya washiriki wanaokidhi vigezo, ili ushindi unaopatikana uwe wa haki.


Pia, ameutaka uongozi wa SHIMMUTA kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika maandalizi na uhakiki wa washiriki, pamoja na kuweka mazingira yanayowezesha wanawake, wanaume na watu wenye ulemavu kushiriki kwa kuzingatia kanuni za michezo.


Amewataka wanamichezo kuheshimu waamuzi na washindani wao, kuzingatia kanuni na kuepuka vurugu, ubaguzi na udanganyifu.


“Timu yako ikifungwa mara hii, wewe omba uzima ije SHIMMUTA nyingine,” amesema, akisisitiza kuwa kushindwa kusiwe sababu ya kuvunja umoja na undugu.


Akizungumzia maandalizi ya AFCON 2027, Waziri Mkuu amewataka Watanzania, hususan watoa huduma, kuwa wakarimu kwa wageni na kutunza miundombinu ya michezo ili iendelee kutumika baada ya mashindano hayo.


Awali, Mwenyekiti wa SHIMMUTA, Marcel Bituro, amesema mashindano hayo yanalenga kuimarisha afya, mshikamano na tija mahali pa kazi. Pia, ameomba wadau kuunga mkono shirikisho hilo kupitia udhamini wa muda mrefu.

 


Wananchi wa kijiji  cha Makhoromba wilayani Karatu hivi karibuni wanatarajiwa kupumua baada ya kumalizika kwa ujenzi wa uzio wa umeme unaofanywa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  ambapo kwa sasa mradi huo  umefikia asilimia 72  ili uweze kukamilika.



Lengo la ujenzi wa uzio huo ni kuondoa migogoro baina ya wanyamapori wakali na waharibifu dhidi ya wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM inayosisitiza umuhimu wa wananchi kulindwa.



Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mamlaka  ya Hifadhi ya Ngorongoro Victoria Shayo, amesema ujenzi huo unafanyika ili wananchi katika eneo hilo na mali zao waweze kuwa salama.



Ziara hiyo imehitimishwa kwa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika kulinda na kutunza mazingira pamoja na kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu kwani uwepo wake utawazuia wanyamapori wakali kutotoka ndani ya hifadhi  ya Ngorongoro.



 


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru jana usiku tarehe 9 Novemba. 2026 alitua kwenye kambi ya timu hiyo inayoshiriki mashindano ya SHIMMUTA mkoani Morogoro kukagua hali ya kambi hiyo na maendeleo ya wachezaji.



Mara baada ya kukutana na wachezaji hao Dkt.Badru*l ametoa maelekezo ya wanamichezo wa Ngorongoro kutumia fursa hiyo Kama mojawapo ya kujifunza mambo mapya kutoka taasisi nyingine.


“Tumieni michezo kuitangaza Ngorongoro, chezeni kwa nguvu zenu zote Ila mkumbuke michezo ni furaha na amani na muwe tayari kupokea aina yoyote ya matokeo,”alisema Dkt.Badru.



Afisa Michezo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Yotham Gitige alimshukuru kamishna kwa ziara hiyo na kusema kuwa imewatia moyo katika ushiriki wao kwenye michezo hiyo.



Waswahili husema Hayawi hayawi sasa yamekuwa na Mwanzo wa Ngoma ni Lele, na sasa Ngoma inachezwa kufuatia Ngorongoro Scholarship Fund iliyozinduliwa tarehe 4 Agosti, 2026 kuwezesha wanafunzi waishio hifadhi ya Ngorongoro kupata fursa ya elimu ambapo wanafunzi 14 wamepatikana na kuagwa leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Vyuo vikuu mbalimbali.



Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa kupitia Ngorongoro Scholarship Fund , NCAA kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo baada ya uchambuzi jumla ya wanafunzi 14 wamekidhi vigezo na kuchaguliwa kujiunga Vyuo vikuu ambavyo ni Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-MWEKA, Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) na chuo Kikuu cha SAUT ambapo wamedahiliwa katika masomo ya u Uhifadhi wa Wanyamapori, misitu, Malikale na utalii.



“ Kupitia Ngorongoro Scholarship Fund tumetenga Milioni 100 mwaka huu kufadhili wanafunzi, tunaamini wanafunzi hawa wakimaliza masomo yao itawawezesha kujiajiri ama kuajiriwa maeneo mbalimbali Serikalini na Sekta binafsi, Utekelezaji wa program hii ni utekelezaji wa majukumu matatu ya Ngorongoro katika uhifadhi, utalii na kuwaendeleza wakazi waishio ndani ya Hifadhi. Ufadhili huu unalenga kusaidia wenyeji wenye sifa za kupata elimu ya vyuo vikuu, mpango huu utatekelezwa kila mwaka kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo kwa kuzingatia muongozo wa utoaji wa mikopo” amesema Dkt. Badru.



Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Dkt. Bill Kiwia ameeleza kuwa kupitia Ngorongoro Scholarship Fund l Bodi hiyo ilipokea maombi 26 na baada ya kuchakata jumla ya wanafunzi 14 walikidhi vigezo na kunufaika na ufadhili huo kwa kuzingatia misingi ya haki, usawa na uwazi kwa wote wanaostahili na kuongeza kuwa kwa wanafunzi 14 waliopatikana jumla ya shilingi Milioni 70.6 itatumika kufadhili gharama za masomo yao ili kutimiza ndoto zao za kupata ujuzi, fursa ya kusaidia taifa katika shughuli za uhifadhi, utalii, mazingira. 



Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Wafugaji  Ngorongoro James Moringe ameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 93 wa Sekondari, wanafunzi 33 wa kidato cha 5 na 6, wanafunzi 36 ngazi ya vyuo vya Kati na wanafunzi 14  waliopata ufadhili wa vyuo vikuu mwaka huu.



Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Ndina Koyaki Mollel kutoka kata ya Alailelai ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kufikia ndoto ya kupata elimu iwe fursa kwao kujiajiri, kuajiriwa na kusaidia familia zao na kuiomba serikali kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa kwa miaka ijayo.

 


Dar es Salaam, Tarehe 6 Novemba, 2026.



Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru amehitimisha safari yake ya udaktari wa falsafa baada ya kufaulu katika hatua ya mwisho ya masomo yake kwa kufanya utetezi wa mwisho  (Viva Voce) kwenye jopo la wasomi na jamuiya ya wadau mbalimbali waliohudhuria tukio hilo kwenye makao  makuu ya *Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tarehe 6 Novemba, 2026.



Chini ya usimamizi  wa Profesa Deus Ngaruko na Dkt.Harriet Mtae Kamishna Badru* alifanya utetezi wa shahada yake ya uzamivu katika mada iliyobeba kichwa cha habari  *Socio-economics Determinants of Housing Affordability for Public Servants in Tanzania:Case of Rent-paying house holds in Dar essalaam* .


Baada ya utetezi na mahojiano ya zaidi ya saa tatu jopo la wasomi lilifanya hitimisho kwa kusema, "Abdul-Razaq Badru umefaulu udaktari wako wa falsafa”,(PhD).


Kamishna Badru atahudhurishwa katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria yatakayofanyika hivi karibuni na hivyo kuanza rasmi safari ya udaktari wa falsafa.


HONGERA SANA  AFANDE BADRU

 


Ataka Serikali na taasisi za dini kuimarisha ushirikiano kwa kuzingatia uzoefu wa sekta ya afya

Hai, Kilimanjaro

WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amemwelekeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kuandaa mpango wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini katika elimu, kwa kuzingatia uzoefu wa ushirikiano uliopo katika sekta ya afya.

Ametoa maelekezo hayo leo, Jumapili, Novemba 1, 2026, wakati akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ibada ya uzinduzi wa nyumba mpya ya ibada ya Bethel ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nshara, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

“Mheshimiwa Waziri, utaenda ukae na wenzako. Kaa na Waziri wa Afya,” amesema Dkt. Mwigulu.

Ameelekeza wataalamu wa wizara hizo kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano katika elimu na kuandaa mpango utakaowasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata ridhaa ya Serikali.

Maelekezo hayo yamefuatia maelezo kuhusu ujenzi wa kampasi ya Machame ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo), kinachomilikiwa na KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, pamoja na ombi la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa katika kutoa elimu.

Akifikisha salamu za Rais, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa taasisi za dini katika maendeleo ya Taifa na itaendelea kushirikiana nazo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema historia ya maendeleo ya Tanzania haiwezi kutenganishwa na mchango wa Kanisa, hususan katika elimu na afya, ambako taasisi za dini zimekuwa zikihudumia wananchi bila kujali imani zao.

“Hauwezi ukayataja maendeleo ya nchi yetu hii kwa ustadi wowote ule bila kutaja mchango wa Kanisa,” amesema.

Dkt. Mwigulu amewapongeza waumini wa Usharika wa Nshara, viongozi wa Kanisa, kamati ya ujenzi na wadau wote waliofanikisha ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada, akisema wamefanya kazi kubwa inayostahili kupongezwa.

ATOA MAELEKEZO KUHUSU UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Kuhusu mazingira, Waziri Mkuu amehimiza wananchi kuchukulia kwa uzito utunzaji wa miti na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amemwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, kufuatilia hoja ya ukataji miti iliyowasilishwa katika ibada hiyo, kwa kushirikiana na viongozi na wadau husika.

Aidha, amemwelekeza Mkuu wa Mkoa kufanyia kazi ombi la kufungwa taa za barabarani katika eneo la kanisa na kufuatilia hoja za miundombinu zilizowasilishwa na Mbunge wa Hai.

MALASUSA ASISITIZA MALEZI BORA NA UPATANISHI

Kwa upande wake, Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Malasusa, amewapongeza waumini na wadau waliofanikisha ujenzi huo, huku akisisitiza umuhimu wa malezi bora, mazungumzo katika familia na upatanishi katika jamii.

SHOO AOMBA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA KANISA UENDELEE

Naye Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, ameomba ushirikiano wa Serikali na Kanisa katika elimu na afya uendelezwe.

Amesema uzoefu huo ni msingi wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), unaolenga kutoa huduma kwa wananchi.

MBOWE AFUNGUKA KUHUSU EKARI 50 ZA ELIMU

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Ujenzi, Mjumbe wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe, amesema wananchi walitenga eneo la ekari 50 kwa ajili ya maendeleo ya elimu na kulikabidhi kwa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini.

Ameeleza matarajio yao ya kuona chuo hicho kinatoa elimu bora inayozingatia sayansi na teknolojia.

Kwa mujibu wa risala ya Usharika wa Nshara, nyumba hiyo ya ibada imejengwa kwa zaidi ya miaka kumi kwa gharama zinazokadiriwa kufikia Shilingi bilioni 6.5 na ina uwezo wa kuketisha waumini 2,000 kwa ibada.

Ibada ya uzinduzi na kubariki nyumba hiyo imeongozwa na Askofu Dkt. Shoo, huku Askofu Dkt. Malasusa akitoa mahubiri.

Kwa habari zaidi kuhusu siasa, elimu, afya, utalii, jamii, kilimo, uchumi na mazingira, tembelea tovuti ya Habari Tanzania Hub: www.habaritanzaniahub.co.tz

 



Vifijo, nderemo na shangwe zilisikika  mara baada ya Emilian Ngatunga na Witness Mshigeni kuhitimisha sherehe za ndoa yao ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.




Wawili hawa ilikuwa chaguo lao la kipekee kwa ajili ya kuanza safari mpya ya maisha yao ya ndoa kufanya  sherehe yao ya harusi katika eneo hili lenye mandhari ya kuvutia ambapo kuliifanya siku yao kuwa ya pekee zaidi, yenye furaha na kumbukumbu zisizosahaulika ambazo watazithamini maisha yao yote.



Wakielezea furaha yao, maharusi hao wameonesha kufurahishwa na uamuzi wao wa kuchagua Ngorongoro kuwa sehemu ya kufungia ndoa yao, wakieleza kuwa walipata uzoefu wa kipekee na usioweza kusahaulika.





“Kiukweli Ngorongoro ni sehemu ya pekee kuhitimisha harusi, mapenzi yetu yamekuwa moto moto kwa kufika hapa ni raha juu ya raha, mahaba juu ya mahaba”, walisema wapendao hao.





Ngorongoro inajulikana sana kutokana na historia yake hasa chimbuko la binadamu wa kale na wengine husema kwamba kutokana na historia yake inawezekana tunda la mti wa kati lililiwa katika eneo hilo.



 


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imezindua kituo maalum cha huduma kwa wateja kwa lengo la kuwahudumia wadau mbalimbali wa Uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii kwa karibu kinachojulikana Kama Wateja Experience Centre.




Akizindua kituo hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo amepongeza menejimenti ya Ngorongoro kwa ubunifu na hatua ya uanzishwaji wa kituo hicho  ili kuboresha huduma kwa wateja, kutangaza mazao ya utalii na kuongeza uzoefu usiosahaulika kwa wateja wanaotembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro.



Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa wateja watakaotembelea  kituo hicho elimu ya Vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro na gharama zake, huduma za vibali vya kwenda hifadhini, fursa za uwekezaji, kuunganisha wadau wa utalii na watalii wakiwa Ngorongoro, kupata mafunzo kwa waongoza utalii kuhusu mifumo ya malipo na vivutio vinavyopatikana,  kupokea maoni na mrejesho wa wadau kuhusu huduma wanazopata Ngorongoro.



Meneja Utalii na Masoko wa SACC, Mariam Kobelo, amesema kufunguliwa kwa kituo hicho ni sehemu ya mkakati wa shirika  kuboresha miundombinu na huduma za utalii ambapo Arusha kama kitovu cha utalii ofisi hiyo itakuwa One Stop Centre ya huduma zote za wageni, ikiwa ni maandalizi ya kupokea maelfu ya wageni wa AFCON 2027.



Kituo hicho kitatoa taarifa kuhusu maajabu yaliyopo Ngorongoro, huduma wanazohitaji kuzijua wateja na jinsi wateja wanavyoweza kuelezea mabadiliko ambayo wanahitaji kuyaona.

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuandaa mpango mkakati wa shirika (CSP)  wa miaka  5 na mpango wa muda mrefu  (LTTP) wa miaka 25 kwa kuzingatia maslahi makubwa ya uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.



Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo katika kikao cha bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka hiyo kinachoendelea jijini Arusha kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za shirika kwa robo ya kwanza kuanzia mwezi Julai hadi septemba katika mwaka wa fedha 2026/2027



Ameeleza kuwa uhifadhi na ikolojia ya Ngorongoro na pori la akiba la Pololeti ni lazima ilindwe kwa nguvu zote kwa kuwa uwepo wake unachangia uhai wa hifadhi nyingine ambapo kwa pamoja huchangia kuongeza na kulinda ajira za watanzania na kupata mapato ya Serikali kupitia wageni wanaotembelea ambapo mapato hayo husaidia kuboresha huduma za jamii na maendeleo ya nchi. 



Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru amesema mpango wa shirika hilo umezingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya serikali kupitia dira ya taifa ya 2025-2050 na ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2025-2030