Taarifa za hivi punde ambazo zimethibitishwa kutoka
vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa, mabaunsa wa CCM wamepiga na
kuwajeruhi watu kadhaa ambao walikuwa kwenye msafara wa Makamu
Mwenyekiti wa chama hicho, Mohamed Shein, wakidhani ni makamanda wa CHADEMA.
Habari zimeeleza kuwa mabaunsa hao wameletwa kwa ajili ya kufanya vurugu, kupiga, kutesa,
kuteka, kujeruhi na kuua wapinzani wa CC, ambapo walengwa ni CHADEMA, kama ilivyo ada ya chama hicho tawala kufanya hivyo
kwenye chaguzi mbalimbali, hususan kinapokuwa kimezidiwa na kupata hofu ya kushindwa, wamepiga na kujeruhi takriban watu 9.
Mabaunsa
hao wakiwa kwenye operesheni ya kile 'walicholetewa' Chalinze, jioni
hii, wamewakuta watu waliodhani kuwa ni makamanda wa CHADEMA katika eneo
la Msoga (kwa bwana mkubwa), wakaanza kuwashushia kipigo kikali, kisha
wapigaji hao wakakimbia.
Katika watu hao 9 waliopigwa na mabaunsa hao wa CCM, wamo maofisa wa UWT, mtoto wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo na waandishi wa habari na
watu wengine ambao hawajafahamika vizuri 'majukumu' yao kwenye msafara
huo ambao leo ulikusanya watu wengi kwa kuwasomba kwa malori kutoka
maeneo mbalimbali kwenda kujaza mkutano wa kufunga kampeni huko Miono.
Pamoja
na kukimbia, mabaunsa hao walikamatwa wakiwa kwenye gari yao aina ya
Land Cruiser 'hard top' ambapo ilipofikishwa kituo cha polisi 'mjini'
hapa, limekutwa na mapanga, marungu, kamba, tindikali na petroli.
Kitu
cha kushangaza katika tukio hilo ni kwamba vijana hao wameachiwa pamoja
na gari lao na silaha walizokuwa nazo, bila kufunguliwa jalada la kesi,
baada ya msemaji wa CCM kufika kituoni hapo na maelekezo maalum.
Waliopigwa na kujeruhiwa, inasemekana wamekimbizwa hospitalini Dar es Salaam, kwa maelekezo maalum pia...
Sasa uharamia umeanza kuwageukia...
Breaking News: MABAUNSA WA CCM WAPIGA NA KUJERUHI MSAFARA WA SHEIN
Sunday, April 06, 2014
No Comment
0 Comments:
Post a Comment