- Mnyika ametaka kutoa hoja juu ya kusitishwa kwa mjadala ili wabunge wapewe nakala halisi ya Hati ya Muungano. Mwenyekiti, Sammuel Sitta amemjibu kuwa awasilishe hoja hiyo Bungeni kwa utaratibu unaokubalika na itajadiliwa.
- Mwenyekiti wa Kamati Namba Mbili, SHAMSI VUAI NAHODHA anawasilisha taarifa ya kamati hiyo. Anasema kuwa mjadala ndani ya kamati ulikuwa mkali
- Nahodha anasema kuwa Ibara zinazohusu Jamhuri ya Muungano, Muundo wa Serikali na Vyombo vya Utendaji vilipitishwa lakini havikupata atheluthi Mbili ya kura hivyo ameleta Bungeni kwa maamuzi
- Shamsi Nahodha anasema kuwa Neno Shirikisho limependekezwa lifutwe kutokana na sababu zifuatazo
- Hati ya Muungano ambayo ndiyo msingi wa muungano wetu haikupendekeza neno Shirikisho badala yake imetumia neno Jamhuri ya serikali mbili
- Shirikisho litahatarisha uhai wa muungano na
- shirikisho litaweka nchi yetu katika hatari ya kuvamiwa wakati wowote
- Kuhusu Ibara ya Pili, Kamati imependekeza kuongeza maneno ya mito na maziwa kama sehemu ya mipaka ya nchi kwa vile nchi yetu ina mipaka ndani ya Bahari, nchi kavu, mito na maziwa
- Kuhusu Muundo wa Muungano, Ibara ya 60(1), Kamati imependekeza muundo wa Serikali mbili ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kamati imependekeza muundo huo kutokana na
- Hati ya Muungano
- Kuweka mgawqnyo sawa wa majukumu ya Serikali
- Kwa jinsi Nahodha anavyowasilisha, maoni ya walio wengi ni kwamba Muundo wa Muungano wa Serikali mbili ndio uliopendekezwa
- MAONI YA WACHACHE YA KAMATI NAMBA MBILI
Maoni ya wengi yamelenga kutaka kupoteza kiini cha Rasimu yenye maoni ya wananchi. Wanasema kuwa kama walio wengi waliona kuwa ni bora kufanya marekebisho ya katiba iliyopo, kulikuwa na haja gani ya kuunda tume ya mabadiliko ya katiba.
- Nawaona Lema na Mtikila wanalalama kuwa taarifa inayosomwa juu ya maoni ya wachache si yenyewe. Hata hivyo, Nahodha amesema kuwa alichokifanya ni kufupisha uwasilishaji ilimkwenda sambamba na muda uliopo. Kwamba ametumia dakika 34 kuwasilisha taarifa ya walio wengi na ana dakika 26 tu kuwasilisha maoni ya wachache. Hivyo kwa vile taarifa yao ni ndefu, ni wazi kuwa hawezi kuwasilisha ndani ya dakika 26 zilizopo. Muafaka umepatikana na Nahodha anaendelea kuwasilisha
- SABABU ZA WACHACHE KUPENDEKEZA MUUNDO WA SHIRIKISH
- Hari ya Muungano inayotumiwa kama reference na walio wengi haina saini za waasisi wa muungano
- wasomi mbalimbali kama vile Prof Haroub Othman na Prof Issa Shivji wao wamesema kuwa muungano uliopo ni wa shirikisho.
0 Comments:
Post a Comment