SHERIA YA KUZUIA UTAKASAJI FEDHA HARAMU YA 2006 SI HALALI- WANASHERIA

MADIWANI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) jijini hapa pamoja na mbunge, Godbless Lema, wamemtaka Mkuu wa wilaya ya Arusha, John Mongela kuacha kuingilia shughuli za utendaji ambazo kisheria ziko chini ya  mkurugenzi wa jiji,Juma Iddi.

 

Aidha wamewataka wamachinga walionyang'anywa mali zao na mgambo wakati wa operesheni safisha jiji, wafike kwenye ofisi za  jiji ambapo wataongoza zoezi la kuwarejeshea mali zao kuanzia majira ya asubuhi muda wa kazi unapoanza.

Pia wamemtuhumu Mkuu huyo wa Wilaya kuhusika na vitendo vya ubadhirifu wa fedha zinazotokana na mapato ya ushuru kwenye masoko mbalimbali ya jiji ambapo tayari suala hilo wamelifikisha kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa nchini, (TAKUKURU).

 

Waliyasema hayo jana wakati wakiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Kibo Palace ambapo walikuwa madiwani wote wa Chadema, akiwemo Naibu Meya, Prosper Msofe, Mbunge Lema na viongozi wa Chama hicho ngazi ya wilaya.

 

Lema alisema kuwa hawapingi  jiji kuwa safi kwani ni agenda ya Chadema na inatekelezwa kwenye maeneo ambayo chama hicho kinaongoza halamshauri ila wanachokataa ni zoezi hilo kutekelezwa kwa ukatili mkubwa huku likishindwa kusimamia misingi ya haki na heshima ya utu.

 

Alisema kuwa wamekaa kama madiwani wameona Mkurugenzi wa jiji anaingiliwa sana kwenye masuala ya utendaji na Mkuu wa wilaya jambo alilodai kuwa linathibitishwa na tukio la hivi karibuni ambapo madiwani na mkurugenzi walikaa na kuamua kuwasimamisha kazi mgambo ili kupisha uchunguzi wa tukio la Diwani Ephata Nanyaro na Naibu Meya, Msofe kupigwa .

 

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alisema kuwa katika hali isiyotarajiwa Mkuu wa Wilaya alienda kwenye vyombo vya habari akawatangazia mgambo kurudi kazini jambo alilosema kuwa si sahihi kwani mgambo wanaajiriwa na mkurugenzi chini ya idara ya sheria hivyo maamuzi ya madiwani na mkurugenzi hayakuwa sahihi kupuuzwa na DC.

 

"Tatizo la wamachinga ni kubwa kuliko watu waanavyofikiria, huwezi kulimaliza kwa siku moja , linahitaji mkakati madhubuti , hapa Arusha tuna maeneo makubwa ambayo ni mali za jiji lakini yaliuzwa kifisadi kama lile lililopo pale pembeni ya soko la kilombero ,Rais anaweza kutumia mamlaka yake kwa kufuta ile hati , eneo lile likatumika kwatengenezea miundombinu itakayowezesha wamachinga wengi kuendesha shughuli zao," alisema Lema.

NAIBU MEYA ATOIA MSIMAMO KUITISHWA BARAZA LA MADIWANI

Kwa upande wake Naibu Meya Msofe, alisema kuwa leo (jumatatu) watamwagiza Mkurugenzi wa jiji, kuitisha kikao cha baraza la madiwani la dharura kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hilo la machinga.

 

Pia amewataka wamachinga kufika kwenye ofisi za jiji kwa ajili ya kuchukua mali zao ambazo mgambo waliwanyang'anya bila kufuata utaratibu, kanuni wala sheria ambapo zoezi hilo litasimamiwa na madiwani wa Chadema.

 

"Sisi kama baraza la madiwani tuliwaagiza mgambo kuzuia watu wasiweka mali zao barabarani lakini hatukuwatuma wakawapige kama wanavyofanya , wananchi wote walionyang'anywa mali zao waje pale halmashauri tutawarudishia," alisema Msofe.

NANYARO ADAI MGAMBO NI WA CCM WAMFIKISHA DC TAKUKURU

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Levelos, Aphata Nanyaro alisema kuwa weanaushahidi kuwa zaidi ya asilimia 95 ya mgambo wa jiji hilo ni kundi la walinzi wa CCM "Green Guard" jambo alilodai kuwa pia linatiwa uzito zaidi na kauli wanazowaambia wananchi mara baada ya kuwapiga na kuwanyang'anya bidhaa zao .

 

"Zoezi la kusafisha jiji pamoja na kuwaondoa  machinga barabarani linaendeshwa tofauti na maazimio ya baraza la diwani, sisi tulisema kuwa lazima liongozwe mwanasheria wa halmashauri, atakayefuatana na watu wa mipango miji pamoja na wale wa idara ya biashara ili kuhakikisha zoezi hiulo linakuwa na ufanisi bila kukiuka sheria na haki za wananchi," alisema Nanyaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema wilayani  hapa.

 

Alisema kuwa kwa sasa kuna malalamiko mengi toka kwa machinga kuwa wamenyang'anywa mali zao na hazijulikani zilipo na wengine wanadai wameona mgambo wamevaa vitu walivyowanyang'anya huku wale wanaouza vyakula wakilalamika bidhaa zao kuharibiwa na nyingine kuchukuliwa bila kuorodheshwa jambo linalowanyima haki .

"Sisi kama madiwani wa Chadema tunaweka wazi kuwa hatutakuwa tayari kufanya kazi na DC (Mongela) kutokana na vitendo vyake vya kuingilia masuala yaliyopaswa kufanywa na Mkurugenzi, na hivi tunavyoongea tumeshapeleka barua TAKUKURU tukianisha tuhuma zake za kula rushwa kwenye masoko ya NMC, Kilombero na Krokoni tili wazichunguze na wamfikishe kwenye vyombo vya sheria," alisema Nanyaro.

MAWAKILI wa utetezi kwenye shauri la utakatishaji fedha haramu linalowakabili washtakiwa wanne akiwemo wakili maarufu, jijini hapa, Median Mwale, wameibua hoja nzito kisheria juu ya uhalali wa kutumika kwa sheria ya kuzuia utakatishaji fedha haramu kwani haijatangazwa kwenye gazeti la Serikali baada ya kusainiwa na Rais.

 

Aidha wanalalamikia wateja wao kufunguliwa mashtaka kwa kutumia sheria zilizoidhinishwa kuanza kutumika baada ya wao kuwa walishakamatwa jambo walilodai kuwa ni kinyume cha sheria.


Pia  wamelalamikia ucheleweshwaji wa makusudi wa kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo unaofanywa na upande wa Serikali kwa kigezo kuwa upelelezi haujakamilika huku wateja wao wakiendelea kuteseka rumande kwa miaka mitatu sasa.

Hayo yamesemwa jana na Wakili wa utetezi, Omary Iddi Omary, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Devota Kamuzora ambapo wakili huyo anashirikiana na mawakili, Mosses Mahuna na Modest Akida huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na Wakili, Tumaini kweka.

Waliiomba mahakama hiyo iridhie ombi lao la kupeleka mkanganyiko huo wa kisheria Mahakama Kuu ili ukapatiwe tafsiri ya kisheriaikiwemo uhalali wa sheria hiyo waliyodai kuwa mchakato wake  una mapungufu kisheria kwani haujatangazwa kwenye gazeti la serikali baada ya Rais kuisaini ili kuiwezesha kuanza kutumika.

Alisema kuwa katiba ya nchi inaelekeza kuwa baada ya bunge kutunga sheria na kuipitishwa muswada huo unatakiwa kuridhiwa na Rais ambapo baada ya hapo unapaswa kutangazwa kwenye gazeti la serikali ndipo ianze kutumika jambo ambalo mpaka sasa sheria hiyo haijatangazwa hivyo si sahihi kisheria kuanza kutumia.

 

"Sheria hiyo iliwekwa kwenye gazeti la serikali Januari 12,
2006 kabla ya kusainiwa na Rais, (Jakaya Kikwete) Januari 15, 2007, ukiangalia tarehe hizo mbili utaona ilitangazwa kabla Rais hajaisaini kuiridhia na baada ya kusainiwa na Rais haijatangazwa ili ianze kutumika hivyo sheria hii haiwezi kuwa halali kutumika mpaka itakapotangazwa.

 


"Mheshimiwa hakimu , kutokana na ukiukwaji wa taratibu hizo, unafanya sheria ya Uzuiaji Utakasaji Fedha Haramu ya mwaka 2006 isiwepo, hii inamaana hata  washtakiwa  hawa wanashikiliwa kwa kutumia sheria ambayo haipo, …hata kosa wanaloshtakiwa nalo halipo kwenye sheria za sasa, katika
mazingira hayo hakuna shaka kuwa hapa hakuna mashtaka sahihi," alisema Wakili Omary.





Hata hivyo alisema kuwa wateja wake ambao mbali ya Mwale wapo, Elius Ndenjembi ,Don Bosco Gichana na Bonifasi Mimbwa wanashitakiwa kwa kutumia sheria mbili jambo alilodai kuwa upande wa Serikali wanataka kuzitumia kama kichaka kuona ni ipi itakuwa na maslahi kwao hasa pale sheria moja itakapoonekana kushindwa basi watumie hiyo nyingine kuendelea kuwashikilia wateja wake.

Omary aliieleza mahakama hiyo kuwa wateja wake wameshitakiwa kwa kosa kosa la kula njama kutenda kosa kinyume cha sheria huku kwenye maelezo ya kosa ikitumiwa sheria nyingine ambapo wanadaiwa kukiuka sheria ya uzuaji utakasaji fedha ya mwaka 2006 jambo alilodai kuwa linakiuka sheria ya uendeshaji mashauri ya jinai, (CPA).

 

Omary aliieleza mahakama hiyo kuwa sababu nyingine inayowafanya kuomba kwenda mahakama Kuu ni kuwa  kifungu kilichotumika kufungua mashtaka ni kile
kilichofanyiwa mabadiliko februari 24, 2012 wakati muda huo tayari wateja wake walikuwa tayari wanashikiliwa mahabusu jambo alilodai kuwa ni kinyume cha sheria.




Akijibu hoja hizo wakili wa Serikali, Tumaini Kweka akijibu hoja hizo alisema kuwa hazina msingi kwa madai kuwa sheria hutumika baada ya kupitishwa na bunge na kuwa imefuata michakato yote ndipo huanza kutumika.



"Nafikiri wameleta malalamiko kwenye eneo lisilo sahihi, kwani hata kwa mujibu wa uanzishwaji wa mahakama hii sidhani kama wewe (hakimu) unaweza kuamua mashauri ya Manyara, hii ni sawa na kumtuma mtoto akachukue chakula cha Mlinzi," alisema Wakili Kweka jambo lilomfanya hakimu kuingilia kati na
kumtaka afute kauli yake hiyo ya kumfananisha yeye na mlinzi.

Hata hivyo wakili huyo aliendelea kusisitiza kuwa shauri hilo lipo
mahakamani hapo kwa ajili ya kuahishwa na kupangiwa tarehe nyingine kwa maelezo kuwa mahakama hiyo haina nguvu kisheria kusikiliza shauri hilo.



Akijibu hoja hiyo wakili wa Washtakiwa, Omary alisema kuwa hata wao wanajua kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza shauri hilo ndiyo maana wanaomba kupewa idhini kwenda mahakama kuu wakapatiwe ufafanuzi wa kisheria juu ya yale wanayoyalalamikia.



Hakimu Kamuzora ameahirisha shauri hilo mpaka Mei 12 kwa ajili ya kutoa uamuzi mdogo .

 

0 Comments:

Post a Comment