DC MONGELA AJIBU


Akijibu madai hayo, Mkuu wa Wilaya, Mongela alisema kuwa madiwani hao hawajui mipaka ya uongozi kwa kile alichodai kuwa suala la usafi ni la watendaji ambapo baada ya madiwani hao kuamua kwenye kikao chao cha baraza la madiwani shughuli hiyo ilibaki kwa watendaji ambao walimuomba kusaidia utekelezaji .

 

"Suala la mgambo ni la kiufundi zaidi, kila halmashauri ina mgambo hata mataifa ya nje yanawatu hawa wa kusimamia sheria ndogondogoi za maeneo husika, mtu anaposema anawasimamisha tutakuwa wa kwanza duniani , hata mimi nimetoka Kigom nimewakuta mgambo," alisema Mongfela kwa njia ya simu.

 

Hata hivyo alisema kuwa haungi mkono mgambo kupiga wananchi na kama kweli wapo waliojeruhiwa basi mgambo hao wachukuliwe hatrua za kisheria kama wahalifu wengine .

 

Hata hivyo alikanusha kujihusisha na ufisadi wa mapato ya ushuru kwenye masoko kwa madai kuwa kwa mfumo wa utendaji ulivyo yeye yuko mbali ingawa alisema kama limepelekwa takukuru ni vema likachunguzwa ili ukweli ujulikane.

 

 

0 Comments:

Post a Comment