NANYARO ADAI MGAMBO NI WA CCM, WAMFIKISHA DC MONGELA TAKUKURU


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Levelos, Aphata Nanyaro alisema kuwa weanaushahidi kuwa zaidi ya asilimia 95 ya mgambo wa jiji hilo ni kundi la walinzi wa CCM "Green Guard" jambo alilodai kuwa pia linatiwa uzito zaidi na kauli wanazowaambia wananchi mara baada ya kuwapiga na kuwanyang'anya bidhaa zao .

 

"Zoezi la kusafisha jiji pamoja na kuwaondoa  machinga barabarani linaendeshwa tofauti na maazimio ya baraza la diwani, sisi tulisema kuwa lazima liongozwe mwanasheria wa halmashauri, atakayefuatana na watu wa mipango miji pamoja na wale wa idara ya biashara ili kuhakikisha zoezi hiulo linakuwa na ufanisi bila kukiuka sheria na haki za wananchi," alisema Nanyaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema wilayani  hapa.

 

Alisema kuwa kwa sasa kuna malalamiko mengi toka kwa machinga kuwa wamenyang'anywa mali zao na hazijulikani zilipo na wengine wanadai wameona mgambo wamevaa vitu walivyowanyang'anya huku wale wanaouza vyakula wakilalamika bidhaa zao kuharibiwa na nyingine kuchukuliwa bila kuorodheshwa jambo linalowanyima haki .

"Sisi kama madiwani wa Chadema tunaweka wazi kuwa hatutakuwa tayari kufanya kazi na DC (Mongela) kutokana na vitendo vyake vya kuingilia masuala yaliyopaswa kufanywa na Mkurugenzi, na hivi tunavyoongea tumeshapeleka barua TAKUKURU tukianisha tuhuma zake za kula rushwa kwenye masoko ya NMC, Kilombero na Krokoni tili wazichunguze na wamfikishe kwenye vyombo vya sheria," alisema Nanyaro.

0 Comments:

Post a Comment