CHUO KIKUU CHA ST JOSEPH CHAZINDUA ELIMU YA MASAFA KWA MTANDAO


 WATOA TABLET KWA WANACHUO 500 BURE












WANACHUO wa  Mt. Joseph tawi la Arusha wakiwaburudisha wageni waalikwa katika sherehe ya uzinduzi wa chuo kikuu hicho.

0013
Katibu mkuu wa wizara ya elimu, Profesa Sifuni Mchome hakiwaonyesha wageni pamoja na wanafunzi Tablets ambazo chuo hicho huwagawia wanafunzi hili ziwasaidie wenye masomo.
0016
 Afisa masoko wa chuo hicho, Recho Jackson akielezea matumizi ya tablet hizo wakati wa hafla hiyo.
0022
Katibu mkuu wa wizara ya elimu, Profesa Sifuni Mchome akimkabidhi mmoja wa wanachuo tablet
0026
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Mt. Joseph wakionyesha tablet alizogawiwa

0007
WANACHUO WA St Joseph wakimsikiliza Katibu Mkuu Prof Mchome
CHUO Kikuu Cha Mtakatifu Joseph, Tawi la Arusha, kimegawa kompyuta aina ya  “tablet” kwa wanachuo 500 wa chuo hicho tawi la Arusha, kwa lengo la kuwapa motisha ya kujisomea zaidi.

Aidha kimezindua masomo kwa njia ya mtandao “Virtual university” huku kikitoa wito kwa shule za sekondari za jijini hapa kutumia maabara za Sayansi zilizopo chuoni hapo bila malipo yoyote.

Hayo yalisema na Afisa Mosoko wa Chuo hicho, Rachael Jackson,wakati wa uzinduzi rasmi wa utoaji elimu kwa njia ya mtandao ulioenda sanjari na ugawaji wa “Tablet” hizo uliofanywa na Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Prof. Sifuni Mchomewa aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.

Alisema kuwa “tablet” hizo zitawasaidia wanachuo kupata taarifa
mbalimbali kutoka kwa wahadhiri wao kuhusiana na masuala ya taaluma,ikiwemo silabasi, vitabu mbalimbali vya taaluma pamoja na kufanya usahili hivyo kuondoa ulazima wa wanachuo hapo kufika chuoni hapo kwa ajili ya kupata taarifa hizo..

“Pia wazazi wataweza kupata taarifa za watoto wao kuhusiana na
taaluma, matokeo ya mitihani, mahudhurio, ada na ratiba ya mihula mbalimbali ya chuo hicho kwa kuangalia kwenye mtandao wa chuo,” alisema Jackson.

Kwa upande wake Katibu mkuu Wizara ya Elimu, Prof. Mchome mara baada ya kugawa “tablet” kwa baadhi ya wanachuo aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuwapa wanachuo wao kompyuta hizo.

Alisema kuwa kwa sasa hapa nchini kuna kuna upungufu wa walimu wa Hisabati na sayansi 26,998, ambapo kwa sasa waliopo ni 14,067 wakati mahitaji halisi inahitajika kuwe na waalimu 41,065.

Prof Mchome alisema kuwa kwa idadi ya wahitimu wa ualimu wa masomo hayo kila mwaka ni 2005 jambo alilodai kuwa linaweza kuchukua zaidi ya miaka 11 kufikia malengo.

Alisema kuwa Wizara yake katika kulipatia ufumbuzi changamoto hiyo imeandaa mchakato utakaowashirikisha wadau wa Elimu ikiwemo chuo hicho kuhakikisha wahitimu wa masomo hayo ambao sio waalimu kitaaluma wafundishe masomo hayo kwa mkataba sanjari na kuajiri waalimu kutoka nchi jirania mahitaji makubwa ya walimu


Kwa upande wake mmoja wa wanachuo wa chuo hicho aliye mwaka wa kwanza, Joseph Namfua alisema kuwa “tablet” hizo zitawasaidia sana kutokana na wahadhiri kuwapa kazi za kuandika kwenye CD hivyo ilikuwa ikawalazimu kuwa na kompyuta.

Tawi hilo la Arusha lilianza kupokea wanachuo kwa ajili ya ualimu kwa masomo ya sayansi mwezi Agosti mwaka jana.

0 Comments:

Post a Comment