MILIPUKO YA MABOMU ILIYOTOKEA KWENYE MABASI MAWILI JIJINI NAIROBI,KENYA YAUA WATU WATATU NA 62 KUJERUHIWA VIBAYA
Monday, May 05, 2014
No Comment
Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 62 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka Jumapili ya leo katika barabara ya Thika, ambayo ni moja ya njia kuu zenye magari mengi jijini Nairobi, Kenya.
Majeruhi 20 kati ya hao wako mahututi.
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya Bw. Moses Ombati amenukuliwa akisema kuwa mabomu hayo yamelipuka kwenye mabasi ya abiria mawili tofauti, ambapo Naibu Mkuu wa kitengo cha kutengua Mabomu, Bw, Eliud Lagat amesema milipuko hiyo imetokana na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.
Milipuko hiyo na maafa hayo yamekuja siku moja baada ya watu wanne kuuwawa kwa mlipuko wa bomu ya kutupwa kwa mkono katika kituo cha mabasi mjini Mombasa.
0 Comments:
Post a Comment