BAVICHA wamewaalika kuchangia damu Jumamosi hii!

*People's ...*

*Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Arusha Mjini linawatangazia Vijana na raia wote wenye mapenzi mema na Taifa letu kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi tarehe 16/09/2017 kuanzia majira ya saa 2:00 asubuhi mpaka saa 4:00 asubuhi katika Hospitali ya Mount Meru - Arusha kwa ajili ya kujitolea damu.*

*Tukio hili litakuwa maalum, kwa ajili ya kulipa damu isiyo na hatia iliyomwagika baada ya tukio la hivi karibuni la kushambuliwa kwa risasi Mh Tundu Antipas Mughwai Lissu (MB) Singida Mashariki, Rais wa TLS, Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni.*

*Tunatoa rai kwa Vijana wote wa Arusha na raia wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.*

*Give Blood,*
*Save life.*
*"Changia Damu,"*
*"Okoa Maisha".*

*Imetolewa na;*

*Kisanyage Innocent J*
*M/kiti BAVICHA (W)*
*Arusha Mjini*
*0767 182 164*
*14-09-2017*

Glory Kaaya
Katibu Bavicha (W)
Arusha Mjin
0767 533 992
14-09-2017

0 Comments:

Post a Comment