BREAKING NEWS: IGP Simon Sirro atembelea Makazi ya Polisi yaliyoteketea kwa moto jana Arusha, Rais Magufuli atoa Million 260


IGP Simon Sirro atembelea makazi ya maafisa Wa Jeshi la Polisi yaliyoteketea kwa moto hapo Jana
 Katika ziara take hiyo yakushtukiza IGP Sirro amesema Tukio hilo ni tukio baya kuwahi kutokea.

Pamoja na mambo mengine alieleza kuwa rais Wa jamuhuri ya muungano Wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Magufuli ametoa fedha Kiasi cha Tsh. Million 260 kwa ajili ya msaada Wa kujenga majengo yaliyoteketea huku jeshi la Polisi kupitia mfuko wake likichangia shilingi Millioni 40 ambazo zimekamilisha kiasi cha Tsh. million 300.

IGP Siro amesema Familia za Maafisa Wa Jeshi hilo waliopatwa na janga hilo pamoja na kupatiwa makazi ya muda ambayo yametolewa na wakala Wa majengo Tanzania TBA pia watapatiwa kila familia kiasi cha Tsh million moja  kwa ajili ya kuanzia maisha.

Aidha  Maneja wa TBA Mkoa Wa Arusha Vikta Baltazari amwakabidhi Nyumba mbili zilizopo Tengeru kwa ajili ya hifadhi ya muda ya Familia za maafisa hao Wa jeshi la Polisi.

0 Comments:

Post a Comment