SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii,(NSSF), mkoani Arusha kuwaburuza mahakamani waajiri 126 kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao inayofikia zaidi ya shilingi bilioni 1.
Meneja Kiongozi wa shirika hilo mkoani hapa, Frank Maduga aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa watawafikisha mahakamani kuanzia oktoba 2, mwaka huu.
Alisema kuwa waajiri hao wameshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa zaidi ya miezi sita ambapo miongoni miongoni mwao yapo makampuni makubwa 14 wanaochangia zaidi ya milioni 50 kwa mwezi.
"Waajiri wote tumeshawapa onyo la mwisho na sasa taratibu za kimahakama zinaendelea mkitaka kuwafahamu mtakutana nao mahakamani junatatu," alisisitiza Meneja Kiongozi huyo ambaye hakuwa tayari kutaja majina ya waajiri hao.
Alisema kitendo cha waajiri kutowasilisha michango kinawaathiri wafanyakazi na wategemezi wao ambao wanakosa sifa ya kuendelea kupatiwa huduma za matibabu na fao la uzazi.
"Pia wako wanachama ambao hadi sasa taarifa zao za kumbukumbu hazionyeshifedhayoyotekatikamuda ule ambao michangohaijawasilishwanahivyokusababisha taharuki na msongo wa mawazo kwawafanyakazi husika," alisema Maduga
Michango hiyo inatokana na makato ya asilimia 10 kutoka kwenye mshahara wa wafanyakazi na mwajiri anapaswa kuchangia asilimia 10 nyingine.

0 Comments:
Post a Comment