BREAKING NEWS: Moto mkubwa umeteketeza nyumba 13 za askari katika eneo la Sanawari jijini Arusha; ambapo watu waliopata madhara ni 44 kutokana na familia hizo 13 na imeelezwa kuwa kwa taarifa za awali chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.
PLAY HII VIDEO FUPI HAPA KUTOKA VOA TV News
.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea majira ya saa moja jioni na kwamba moto huo haujaleta madhara yeyote kwa binaadamu bali ni mtu mmoja amepoteza fahamu kwa mshituko.
Amesema katika nyumba hizo 13 askari wanaoishi humo wengine wanafamilia na wengine bado hawajaoa; lakini juhudi zinafanywa ili kuhakikisha kuwa familia hizo zinakuwa salama.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amelipongeza jeshi la polisi kikosi cha zimamoto kwa juhudi za kukabiliana na moto huo; na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea
0 Comments:
Post a Comment