RAIS wa chama cha Wanasheria Tanganyika,(TLS), Tundu Lissu, ametuma ujumbe mzito kwa wanasheria nchini.
Amewata wasikate tamaa katika kupigania haki na kupaza sauti kutetea wanyonge.
Ujumbe huo alimpatia kaka yake, wakili Alute Mughwai alipozungumza naye kwa njia ya simu muda mfupi kabla hajaingia ukimbini hapo ambapo alimhakikishia afya yake imeimarika zaidi ingawa ana maumivu katika majereha ya risasi katika eneo la nyonga na miguuni.
“Jambo la kushangaza na kutia faraja ni kwamba mvumo wa sauti yake ni ule ule wa Lissu anayejulikana na wengi wetu, ujasiri , hamasa na kujiamini hakujaodoka. Ameniambia piganieni haki zenu na haki za watanzania, piganieni uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa maoni na hakikisheni kuna kuwa na demokrasia na utawala wa sheria katika Tanzania” alisema Mughwai akimnukuhu Lissu na kuongeza.
“Rais wetu ufahamu wake umerudi katika hali ya kawaida, anajieleza vizuri maana yake ni kuwa eneo lote la kiunoni kwenda kichwani yuko sawa isipokuwa kuanzia kiunoni kwenda miguuni ndilo eneo lililoumizwa sana.
0 Comments:
Post a Comment