Mahakama yatoa onyo kesi ya Harbinder Sethi

Image result for seth wa iptl
Ijumaa, September 29, 2017 Upande wa utetezi umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuta kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi na mwenzake kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutekeleza amri ya kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kutibiwa.
Katika kesi hiyo, mbali na Sethi mshtakiwa mwingine ni James Burchard Rugemarila ambao wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwemo kutakatisha fedha
na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Kutokana na hatua hiyo, Mahakama imeamuru mshtakiwa Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Muhimbili ndani ya siku 14 na endapo itashindikana Mkuu wa Gereza la Segerea ambalo Sethi yupo, ataitwa mbele ya Mahakamani kuhojiwa kwa kushindwa kutekeleza amri hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Baada ya kutolewa maelezo hayo, Wakili wa Sethi, Joseph Makandege aliiambia Mahakama kuwa kumekuwepo na mfululizo wa amri za Mahakama zikiagiza mteja wake apatiwe matibabu na uchunguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Hakimu Shaidi alisema pamoja na amri za Mahakama kuwa hazijatekelezwa, kupitia Swai kukiri kuwa hazijatekelezwa na ni lazima amri za Mahakama zifuatwe.
Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi October 13, 2017 na kwamba hadi siku hiyo Sethi awe amekwishapata matibabu na iwapo atakuwa hajapata Mkuu wa Gereza alilopo afike Mahakamani kujieleza.

0 Comments:

Post a Comment