Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari Leo wakizungumza na waandishi wa Habari kwenye ofisi za Mkoa ya CHADEMA zilizopo Ngarenaro
Mbunge Nasari alisisitiza kuwa kinachofanyika ni kununuliwa kwa madiwani wao na siyo kama inavyosemekana kuungwa mkono utendaji wa Rais.
Nasari amesema anao uthitisho wa picha za video zinazowaonyesha wateule wa rais mkoani Arusha wakipanga mipango ya kuwapa rushwa ya fedha, ahadi ya kazi na makazi ya kuishi madiwani wa chadema ili wakihame chama hicho na kurejea ccm
Katika hatua nyingine Mbunge Nasari amesema yupo tayari kumkabidhi ushahidi huo Rais Magufuli hadharani kama ilivyokuwa kwa ripoti ya Makinikia.
Video hizo amedai kuwa zinawaonyesha baadhi ya wateule wa serikali wakilaumiana kwa kufanya hujuma ya kuchoma shule mkoani hapo mwaka uliopita kwa lengo la kumuhujumu aliyekuwa mkuu wa mkoa wakati huo Felix Ntibenda ambaye aliondolewa baada ya matukio matano ya shule kuchomwa mkoani hapa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.
.. Video inakujia Soon.
Video ya VOA TV News








0 Comments:
Post a Comment