Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Ri Yong Ho amemkosoa Rais Donald Trump wa Marekani kwa kumuita Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuwa ni "Mtu wa roketi".
Kwenye hotuba yake aliyoitoa jana Jumamosi kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa waziri huyo alisema Rais Trump alijaribu kukashifu hadhi ya mamlaka ya Korea Kaskazini. Waziri huyo alisema kwa kufanya hivyo, Trump amefanya kosa lisiloweza kurekebishika litakalolazimisha roketi za Korea Kaskazini kurushwa kwenye eneo lote la Marekani bara.
Waziri Ri aliongeza kwa kusema kama Marekani na majeshi ya vibaraka wake wataonyesha dalili yoyote ya kufanya shambulizi la kijeshi, basi nchi yake itachukua hatua za kushtukiza za kikatili kama mbinu za kujilinda.
Waziri huyo aliita nchi yake kuwa ni taifa lenye silaha za nyuklia. Akaendelea kusema uwezo wa nyuklia wa nchi yake kwa nia zote na sababu zote ni nguvu za kujilinda dhidi ya vita kwa kumaliza tishio la nyuklia la Marekani.

0 Comments:
Post a Comment