Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa- UNSC, limetoa taarifa inayoshutumu shambulio la hivi karibuni la Korea Kaskazini ikiliita shambulio hilo kuwa ni uchokozi wa hali ya juu.
Baraza hilo lilifanya mkutano wa dharura jana Ijumaa kufuatia Korea Kaskazini kurusha kombora lililopita kwenye anga la kaskazini mwa Japani na kudondoka kwenye Bahari ya Pasifiki.
Balozi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa Tekeda Alemu aliongoza majadiliano hayo na baadaye kutoa taarifa. Taarifa hiyo ilisema nchi zote wanachama zinapaswa kutekeleza kwa ukamilifu na kwa haraka maazimio yote muhimu yaliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Taarifa hiyo pia imeelezea nia ya baraza hilo katika kufikia maafikiano kwa njia ya amani, kidiplomasia na kisiasa katika utatuzi wa suala la linaloihusu Korea Kaskazini. Ilisema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakaribisha juhudi za nchi wanachama pamoja na mataifa mengine, kuratibu kufikiwa maafikiano ya amani ya wigo mpana kupitia majadiliano.

0 Comments:
Post a Comment