ALICHOSEMA LEMA BAADA YA WAKILI WAKE KUJITOA

Lema aliiomba mahakama kumpa muda wa kutosha kumpata wakili anayemuamini huku akidai kunaweza kuwa na mitazamo tofauti juu ya kujitoa kwa wakili wake wakati huu hasa mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akiwa kitandani kwa kushambuliwa kwa risasi.

Hata hivyo Hakimu Kamugisha alimkatisha asiendelee na hoja hiyo hivyo Lema akaendelea kusisitiza kuwa endapo atakosa wakili anayemuamini atasimama peke yake mahakamani kujitetea.

Aidha Lema alijaribu bila mafanikio kuikumbusha mahakama kuwa hana imani na hakimu huyo ambaye alimkatisha kwa kumweleza kuwa hayo yalishaamuliwa.

Awali Lema anadaiwa Oktoba 23 Mwaka jana  katika mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa, Lema  alitoa maneno kuwa; “Kiburi cha Rais kisipojirekebisha, Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, Mwaka 2020 haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake.”

“Rais ana kiburi, Rais kila mahali watu wanaonewa,wafanyakazi wa serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amani,watu wananyanyaswa.”Lema alinukuliwa na  Wakili wa Serikali, Mtenga.

0 Comments:

Post a Comment