HABARI KUU: Hizi zaweza kuwa Sababu za Diwani Ngowi kukihama CHADEMA?

Diwani aliyejiuzulu kutoka Chadema nakuhami CCM Grayson Ngowi

 Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimandolu kupitia Chadema  Grayson Ngowi, Ameingia katika Malumbano Mazito na mama Mwenye nyumba Mara baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba kwa mwaka moja na miezi Mitatu kiasi cha shilingi millioni Tatu  na Laki sita pamoja na  kumtapeli Sofa seti ya kijana wake ikiwa ni zawadi ya Arusi .
Mama anaedai kuzulumiwa.
Akizungumza na vyombo vya habari kwa masikitiko makubwa Mama mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina la Mama Hendry amesema diwani huyo ambaye ni mchungaji amemtesa kwa muda mrefu na kodi yake Mama huyo ameleza kuwa Mchungaji huyo alipewa notisi ya kuhama katika nyumba yake ya miezi minne kuisha amegoma kuhama na pia kugoma kulipa fedha zake mpaka sasa Amesema mchungaji huyo ni tapeli kwani amekuwa akimpa ahadi za mara kwa mara kulipa fedha zake lakini  amekuwa akimzungusha kulipa fedha zake Sikuchache mchungaji huyo aliyejivua udiwani kwa tiketi ya Chadema na  kutimkia Ccm mbele ya Rais Magufuli katika uwanja wa mpira shekh Amri Abed Stadium Arusha .

Mama huyo ameomba msaada kwa viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa  wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro kuingilia kati kwani mchungaaji huyo alikuwa kiongozi   mwenzao na sasa sio tena na kama kuna kiongozi aliye karibu naye amsaidie kwani amesikia amenunuliwa anapesa hivyo amlipe kodi yake

Sababu Alizoeleza Diwani Ngowi wakati akijiuzulu Play hii Video hapa

0 Comments:

Post a Comment