![]() |
| Mh. Johnson Mahoma Mgombea Udiwani ACT-Wazalendo - Kata ya Muriet |
Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC nchini Tanzania Imetangaza kufanyika uchaguzi Wa Marudio katika kata ya Muriet Jijini Arusha.
Uchaguzi Wa kata ya Muriet unarudiwa kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Credo kupitia chama Cha upinzani CHADEMA huku akieleza sababu ya madai ya kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli .
Leo HabariTanzaniaGraceMacha.com & VOA TV News imempata Mgombea udiwani Kata ya Muriet Jijini Arusha Bw. Johnson Mahoma kupitia ACT Wazalendo ambaye ameeleza mikakati na ilani ya chama chacke kuelekea uchaguzi huo wa marudio.
Johnson Mahuma ameeleza malengo yake ya kugombea katika uchaguzi huu wa Marudio ikiwa ni pamoja na kusimamia miradi ya wananchi huku suala kubwa ikiwa ikiwa changamoto kubwa ya umeme katika kata ya Muriet, Uhaba wa huduma ya maji, Vituo vya afya na masuala ya elimu.
"Tatizo la umeme ni tatizo sugu katika Kata ya Muriet japo ni sehemu ya jiji la Arusha .. Tatizo la umeme litakwisha katika kata ya Muriet..." Johnson Mahoma
Mahoma amesema kata ya Muriet inakabiliwa na matatizo mengi hivyo ni jukumu la Wana Muriet kumchagua yeye kwa usuluhishi wa Matatizo yanayoikabili kata hiyo.


0 Comments:
Post a Comment