CHMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA
KANDA YA KASKAZINI
(Tanga, Kilimanjaro, Arusha & Manyara)
TAARIFA KWA UMMA
WAGOMBEA WA UDIWANI - KANDA YA KASKAZINI
Tarehe 26 Oktoba 2017, wagombea wafuatao walipitishwa na TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) kwa marudio ya uchaguzi mdogo katika maeneo ya kata mbalimbali zilizopo kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA.
Wagombea hawa wote wamepita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Aidha, chama kina matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.
Jumla ya KATA zitakazokuwa na uchaguzi ni 16, Mkoa wa Tanga ukiwa na kata 3, Mkoa wa Kilimanjaro kata 4, Mkoa wa Arusha kata 8 na Mkoa wa Manyara kata 1.
Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:
Na.
|
MKOA
|
JIMBO
|
KATA
|
JINA LA MGOMBEA
|
1
|
Arusha
|
Arusha Mjini
|
Muriet
|
Simon Moses Mollel
|
Monduli
|
Moita
|
Lobulu Lerango Kivuyo
| ||
Arumeru Magharibi
|
Musa
|
Eliud Loomon Laiser
| ||
Arumeru Mashariki
|
Ambureni
|
Dominick E. Mollel
| ||
Makiba
|
Joyce Ruto
| |||
Maroroni
|
Asanterabi Lazaro Mbise
| |||
Leguruki
|
Rabiel Fanuel Mbise
| |||
Ngabobo
|
Emmanuel Fanuel Salewa
| |||
2.
|
Kilimanjaro
|
Hai
|
Machame Magharibi
|
Elibariki Lema
|
Mnadani
|
Ezra John Nyari
| |||
Weruweru
|
Moses Josephat Kalaghe
| |||
Moshi Mjini
|
Bomambuzi
|
Heldaki Verelian Minde
| ||
3.
|
Tanga
|
Mlalo
|
Lunguza
|
Josia Shemeta
|
Bumbuli
|
Mamba
|
Jafari Ndege
| ||
Korogwe Mjini
|
Majengo
|
Abdalah Khalid Maonga
| ||
4.
|
Manyara
|
Hanang
|
Nangwa
|
Yohana Baha Dafi
|
Katika marudio ya uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana tukiwa na uhakika kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao. Tumezingatia uwezo wa wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana na kuwatumikia wananchi na dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za wananchi.
CHADEMA Kanda ya Kaskazini tunawakumbusha na kuwahamasisha wananchi kushiriki na kufuatilia kampeni na wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kurasiku ya tarehe 26 Novemba 2017, aidha tunalitaka jeshi la polisi lifanye kazi yake kwa weledi bila kuonekana linapendelea chama fulani, sambamba na wasimamizi wa uchaguzi (TUME) kusimamia uchaguzi kwa misingi ya HAKI. CHADEMA Kanda ya Kaskazini haitavumulia uhuni, jinai au matendo yoyote wakati wa kampeni na siku ya uchaguzi yatakayotendwa na YOYOTE kwa nia ya kuvuruga kampeni au kuharibu kile wananchi walichokiamua kupitia sanduku la kura.
Imetolewa leo tarehe 27 Oktoba 2017.
Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini
golugwa@gmail.com
0 Comments:
Post a Comment