HABARI: Diwani wa Kibosho Magharibi Deo Mushi atoa msaada kwa wazee , wanafunzi wasiojiweza, na kufadhili michezo

HABARI: Diwani wa kata ya Kibosho Magharibi Deo Mushi amefanya mkutano Wa Hadhara nakuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata hiyo iliyoko katika Halmashauri ya Moshi vijijini.

Habaritanzaniagracemacha.com & VOA TV News imekuletea Full Story kutoka Moshi.

Mkutano huo uliokuwa na Lengo la kuwaeleza masuala kadhaa ya Maendeleo katika kata hiyo Ulihudhuriwa pia na waalimu wa shule za Msingi na Sekondari, waratibu wa Elimu kata na viongozi wengine waandamizi katika maendeleo ya   Kibosho Magharibi.

Nyanja ya elimu ilikuwa kipengele cha muhimu zaidi katika mkutano huo wa Hadhara.. Katika Kuona hilo Diwani Mushi aliwapatia wanafunzi wanaotoka katika familia/Kaya maskini yaani kaya ambazo hazina uwezo.

Aidha Diwani huyo pia alitoa msaada mwingine wa Masweta kwa wazee ili kujikinga na baridi, Jezi za michezo ya Mpira wa miguu kwa Timu kadhaa za kata hiyo pamoja na mipira kwa shule zote za msingi katika kata ya Kibosho Magharibi.

Deo Mushi aliyelakiwa kwa shangwe na bashasha akiwasili amewapatia watoto hao Daftari tatu kila mwanafunzi na kalamu  ambapo amesema huduma hiyo itakuwa ni endelevu kwa wanafunzi hao.

Mhadhara huo pia ulihudhuriwa na Diwani wa Kata ya Mawenzi Manispaa ya Moshi Bi. Hawa Ali Mushi ambaye pamoja na mengine alipongeza jitihada za Diwani Mwenzake Deo Mushi.



Hapa chini Kuna Video kutoka VOA TV News Tazama .

0 Comments:

Post a Comment