Kila Alhamisi ya October kila mwaka kunafanyika cliniki ya Jicho duniani.
Cliniki hii ya Jicho huwajumuisha watu Wa rika zote wakiwemo vijana, wazee, watoto nakadhalika.
Katika Mkoa wa Arusha Shuflghuli hiyo imefanyika katika Makumbusho ya azimio ya Arusha. Ambapo zaidi wamehudhuria idadi kubwa ya wazee kutoka katika maeneo ya jiji La Arusha.
![]() |
| Diwani wa kata ya Kaloleni Mh. Emanuel Kessu |
Diwani wa Kata ya Kaloleni Mh. Emanuel Kessy amepongeza kufanyika kwa shughuli hiyo katika Kata take huku akisisitiza kuwa huo uwe ni utaratibu wa kila Mara.
Cliniki ya Macho inayofanyika kila alhamisi ya October kila mwaka hufanyika Bure. Nalufadhiliwa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali ambapo shuguli hiyo imefadhiliwa na Lions Club kwa Mkoa wa Arusha nakuwaletea wazee huduma hii bure kwakufanyiwa vipimo vya macho , kupatiwa miwani, dawa na maji.
![]() |
| Uongozi wa Arusha Lions Club |
Akizungumza wakati wa vipimo hivyo Rais wa Lions club Arusha Lion Hussein Amesema wao kama wadau wa maendeleo jukumu lao ni kushirikiana na Serikali kwakufadhili baadhi ya Huduma kwa jamii ya wazee ikiwemo vifaa vya vipimo vya macho, Dawa , Kuwapatia Miwani nakugawa maji kwa wote wanaofika kupatiwa huduma hiyo ili kufikia azma ya pamoja ya kuepuka maradhi yasiyo ya lazima.
![]() |
| Doctor Bennett C Msovu Mratibu wacho Mkoa wa Arusha kutoka Hospitali ya Mount Meru |
Doctor Bennett C Msovu ni mratibu wa Macho Hospitali ya Mkoa wa Arusha katika hospitali ya Mount Meru amesema kila mwaka huo ni utaratibu wao kufanya huduma ya afya ya Macho hivyo wagonjwa wa macho wanaopimwa na kubainika basi hupatiwa miwani , dawa na ushauri.






0 Comments:
Post a Comment