TAHARUKI imewakuta wananchi walikuwa kwenye viwanja vya mahakama Kuu Kanda ya Arusha, wakati polisi wakiwakamata wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu mara baada ya mahakama kuwaachia huru.
Walikamatwa muda mfupi baada ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, David Mrango, kuwaachia huku akisisitiza kama maombi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) yana nia njema basi washitakiwa hao waachiwe huru wasikamatwe tena.
Aidha aliyekuwa mshitakiwa, Elias Ndejembi ndiye alikuwa wa kwanza kukamatwa kwani mara baada ya uamuzi huo alitoka nje ya jengo la mahakama ambapo alitokea FFU mmoja na kumshika.
Hali hiyo iliwafanya mawakili kumuuliza askari huyo anamkamata kwa kosa gani na kama anajua uamuzi ulitolewa na mahakama wa kuzuia washitakiwa hao wasikamatwe.
Hata hivyo idadi ya askari wa kutuliza ghasia, (FFU) iliongezeka wakiwemo waliovalia kiraia hivyo kuanza kumvuta mshitakiwa huyo kuelekea kwenye gari ya polisi aina ya Land rover yenye namba za usajili PT 1222.
Mke wa Ndejembi, Imelda aliamua kupigwa picha namna polisi wanavyovutana na mume wake ambapo polisi waliamua kumnyang'anya simu yake na yeye kuanza kulia huku akimng'ang'ania polisi aliyevaa kiraia amrudishie.
Polisi huyo alikerwa na hali hiyo hivyo kuwaagiza polisi kumkamata na kumpakia kwenye gari hilo ambapo askari hao WA kiume walimpandisha kwenye gari hilo hivyo kuwaweka chini ya ulinzi pamoja na mume wake.
Aliyekuwa mshitakiwa, Don Bosco Gichana raia wa Kenya baada ya kuona hali hiyo aliamua kukimbia akafanikiwa kuruka uzio wa mahakama na kukamatwa na polisi maeneo karibu na hoteli ya kitalii ya Mount Meru
Kwa upande wake wakili Mwale alikamatwa karibu na jengo la mahakama ya biashara na kuingizwa kwenye gari aina ya Land Rover yenye namba za usajili T 953 CSZ pamoja na Boniface Mwimbwa.
Magari hayo yaliondoka mahakamani kuelekea kituo kikuu cha polisi
Nitaendelea kuwahabarisha yanayojiri

0 Comments:
Post a Comment