WAKILI MWALE NA WENZAKE WAACHIWA HURU


Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imewaachia huru wakili maarufu jijini Arusha, Median Mwale na wenzake watatu huku ikimtaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPD)  kutowakamata tena.



Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea, David Mrango baada ya mawakili wa utetezi kwenye shauri hilo kuiomba mahakama isikubali maombi hayo kwani yamelenga kuwatesa wateja wao kwani si mara ya kwanza wameachiwa kishan kukamatwa tena.

Jaji Mrango alisema mahakama haina mamlaka ya kukataa maombi hayo ya DDP ila akasisitiza kuwa endapo wameyawasilisha kwa nia njema basi waondoe shauri hilo na washitakiwa hao wasikamatwe.

Wakili wa utetezi, Albert Msando jana akiwasilisha pingamizi hilo aliieleza mahakama kuwa DPP alitakiwa kutoa sababu za kutokuendelea na kesi hiyo kwani walikuwa na muda wa miaka miwili kufanya hivyo lakini hawakuwa ya Jambo alilodai kuwa kinachofanyiia  ni matumizi mabaya ya sheria.

DPP ameanda polisi  ndani na nje ya mahakama waliovalia sare na ambao hawajavalia sare na magari hapo nje ili wakiondoa hii kesi,wawakamate watuhumiwa na kuwafungulia tena kesi upya,"alisema na kuongeza


"Tangu Agosti 2011 watuhumiwa hawa hawajawahi kuwa nje ya gereza labda wakiletwa mahakamani na hii siyo mara ya kwanza DPP kuondoa kesi na kufungua upya.Tunataka haki hivyo kesi hii isikilizwe kwani sheria haipaswi kutumika kuadhibu watuhumiwa kama wanavyofanya sasa,kuwanyanyasa watuhumiwa,"


Akijibu hoja hizo  wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya,alipinga hoja hizo kwa madai sheria haimlazimishi DPP kutoa sababu ya kuondoa kesi mahakamani pindi akiona kuna haha ya kufanya hivyo.

Kwa upande  madai ya Wakili wa utetezi kuwa DPP ameandaa polisi ili wakiondoa kesi hiyo washitakiwa  wawakamate tena alisema haiwezi kujibu hoja hiyo kwani inahitaji ushahidi.


Hii ni kara ya pili kwa DPP kuondoa shauri hilo mahakamani ambapo Novemba 23 mwaka 2015,shauri hilo liliondolewanna washitakiwa hao kukamatwa na polisi na kufunguliwa kesi upya.

Wakili Mwale na wenzake, Don Bosco Gichana raia wa Kenya, Boniface Mwimbwa na Elias Ndejembi, wanakabiliwa na mashtaka 44 yakiwamo ya utakatishaji fedha haramu, kughushi nyaraka na kukutwa na mali zilizopatikana kwa njia za uhalifu ambapo shauri hilo likifika mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mwaka 2011.


0 Comments:

Post a Comment