UNDANI WA MNYETI JUU YA UNUNUZI WA MADIWANI

MKUU WA Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti amekiri kuwanunua madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) na kutangaza dau kwa madiwani waliobaki pamoja na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

Ametoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyikia  Kata ya Sambasha wakati  ambao Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, (TAKUKURU), wakiendelea na uchunguzi baada ya mbunge wa Nassari kuwakabidhi ushahidi wa  picha za video na sauti kama uthibitisho wa madai ya madiwani kununuliwa.

Jumla ya madiwani sita wa chadema wametimkia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) wakidai ni kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli ambapo septemba 22, mwaka huu  baadhi ya madiwani hao walipata fursa ya kupeana mkono na Rais kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid alipoongea na wananchi baada ya kutunuku nishani maafisa usu WA Jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ).

Jana Mnyeti alisisitiza kuwa serikali imewanunua madiwani hao na ina mpango wa kuwanunua madiwani 20 ili halmashauri hiyo iwe iongozwe na CCM.

 Mnyeti alito msimamo huo akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Arumeru alisema kwamba serikali ina fedha za kuwanunua madiwani wote na hivyo diwani yoyote aliye tayari kununuliwa anakaribishwa kwa kuwa fedha za kuwanunua bado zipo za kutosha.

 “Moja ni hili la madiwani kununuliwa inasemekana walionunuliwa wako sita bado hawajatosha, tunahitaji kununua madiwani 20  ili wawe 26 na turudie kata zote," alisema Mnyeti na kuongeza.

“Kwa hiyo na wale ambao wako tayari kununuliwa pia na wao tunawakaribisha fedha tunazo na tuko tayari kuwanunua na mwisho wa siku tunataka halmashauri yote iwe chini ya CCM,".

0 Comments:

Post a Comment