WATU 12 wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria ya shirika la Coastal, aina ya Cessna Grand Caravan kuanguka kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, (SENAPA).
Ndege hiyo ilianguka karibu na uwanja wa ndege wa Lobo jana majira ya saa 8:30 mchana ambapo watatu walijeruhiwa wakiwemo abiria wawili na rubani ambao majina yao hayajaweza kupatikana mara moja.
Taarifa iliyotolewa na kampuni ya Coastal inasema kuwa majeruhi hao wanapatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya.
Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni mvua iliyokuwa ikinyesha hivyo hapakuwa na uwezekano wa kuona vizuri.
"Wakati anajaribu kutua akajikuta ameshafika katikati ya uwanja akaona hataweza kusimama kabla ya kuumaliza. Akajaribu ku take off pia ikawa late. Alipitiliza uwanja akagonga mti na mawe," ilisema taarifa ya kampuni hiyo.


0 Comments:
Post a Comment