BREAKING: Viongozi na wafuasi 12 wa CHADEMA waendelea kusota polisi, Katibu wa Chama hicho mkoani Arusha anena mazito..

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure 
Mapema Leo tumekuripotia Habari kuhusu Taarifa za kukamatwa Katibu wa mbunge Na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Kisanyage Innocent Mkoani Arusha.

Usiku huu tumempata Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure ambaye amekuwa akifuatilia kinagaubaga hiki cha kukamatwa kwa wanachama kumi na mbili Na gari la Matangazo la chama hicho.


Tazama Video kutoka VOA TV News hapa chini Akizungumza Mh. Elias Mungure
Aidha VOA TV News na Habaritanzaniagracemacha.com ikalazimika kumtafuta Mwanasheria wa Chama hicho kikubwa na cha upinzani Nchini Tanzania Kanda ya Kaskazini Bw. James Lyatu ambaye ametanabaisha suala hili kwa mithili ya kisheria imekaaje.

Bw. James aiambia Habaritanzaniagracemacha.com kuwa wafuasi wa CHADEMA wanaoshikiliwa na maafisa wa polisi hawakutakiwa kukamatwa wenyewe walipaswa kukamatwa pamoja na wale wa chama shindani cha CCM kwani walikuwepo eneo la Tukio.

Katika Hatua nyingine Mwanasheria huyo wa CHADEMA amesema bado utaratibu wa kuwawekea mdhamana wafuasi wao unaendelea hivyo wanachama wa chama hicho wasiwe na wasiwasi.

Aidha pamoja na kukamatwa Wanachama hao wa CHADEMA ambao walisemekana kufanyiana vurugu na wanachama wa chama tawala CCM wanachama wa CCM hawakukamatwa.

VOA TV News ililazimika kwenda hadi makao makuu ya Jeshi la polisi Arusha kuhoji iwapo kama Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo atathibitisha kukamatwa wananchi hao na je kwa nini walikamatwa wafuasi wa CHADEMA pekee? Kwa nini wasingekamatwa na wale wa CCM?

Jitihada za kumpata RPC zikagonga mwamba ambapo hata katika simu haikufanikiwa kwani alikuwa hapokei simu tuliyoipiga kwa zaidi ya Saa 3 mfululizo.

Hapa kuna listi ya Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wa chama hicho wanaoshikiliwa polisi.
1.Kisanyage Innocent - Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini.

Wengine ni wafuasi wa chama hicho

0 Comments:

Post a Comment