CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za mitaa nchini, (TALGWU), kimesema kuwa wataenda mahakani kupata tafsiri ya sheria endapo Serikali haitawarejesha kazini wanachama wao 2,490 iiliyowafukuza kazi kwa kuwa na elimu ya darasa la saba ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa.
Aidha wamemtaka hazina kulipa mishahara ya watumishi wote wa Serikali ili kuwaondolea kero wanachama wao wanaolipwa mishahara kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri ambao wamekuwa wakicheleweshewa hivyo kuwafanya wakatiwe huduma za matibabu kupitia mfuko wa bima yanafya, (NHIF) kwani michango yao haiwasilishwi Kwa wakati pamoja na mifuko ya jamii.
Katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Mtima aliyasema hayo jana aliwasilisha wakati akitoa maazimio ya kikao cha kamati tendaji kilichofanyika siku mbili kwa waandishi wa habari ambapo aliwataja walioathiriwa na zoezi ni watendaji wa vijiji, mitaa na Kata ambao ndiyo wengi pamoja na watumishi wa kada nyingine wakiwemo wanapatiwa sekta ya afya na. ujenzi
Alisema wakurugenzi wa halmashauri waliwaondoa wanachama wao kimakosa kwani maelezo yaliyotolewa na katibu Mkuu wa menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora yalielekeza kuondolewa wafanyakazi waliogushi vyeti lakini wao wakaamua kuwaondoa Wafanyakazi wenye elimu ya darasa la saba.
Mtima alisema kuwa sheria, kanuni na taratibu hazikufuatwa wakati walipowasimamisha kazi watumishi hao wakiwa wamefanya kazi mpaka tarehe 20 kisha wakawaondoa kazini bila kuwalipa.



0 Comments:
Post a Comment