![]() |
| Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Arusha Elias Mungure wakuiongea na vyombo vya Habari hivi punde Arusha |
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh. Freeman Mbowe amesema chama hicho kimesusia uchaguzi huo wa Marudio kwenye kata zote za jimbo la uchaguzi la Arumeru Mashariki kata hizo ni pamoja na Makiba , Maroroni , Ngabobo , Leguruki na Ambureni.
Mbowe amesema chama hicho kinaitaka Tume ya Taifa ya uchaguzi kuitisha kurudiwa uchaguzi tena kwenye kata hizo za Arumeru Mashariki.
chaguzi kwenye kata hizo zimeharibika kwa sababu mbali zilizoelezwa na Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Arusha kupitia kwa Katibu wa chama hicho Mkoa Elias Mungure ambaye amesema kumekuwa na Dosari nyingi ikiwemo vitendo viovu vinavyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwatoa nje mawakala wa chama hicho,
Matatizo ya barua za utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi msimamizi Mkuu wa uchaguzi nazo zimetajwa kuwa Changamoto zilizopelekea chama hicho kususia uchaguzi huo.
Vitendo vya kihalifu dhidi ya Wafuasi na mawakala wa chama hicho navyo vimekuwa sababu nyingine ambapo ushahidi wa video umeonesha mmoja wa viongozi wa chadema tawi la Makiba akikatwa kikatili kwa mapanga na watu waluodaiwa kuwa ni wafuasu wa CCM.
Hadi hivi sasa Habari Tanzania imefanya jitihada za kuntafuta Mkurugenzi wa Arusha DC ambaye ndiye anasimamia uchaguzi kwenye jimbo hilo suala ambalo halikufanikiwa kutokana na Mkurugenzi Huyo kutokupokea simu. Jitihada kumtafuta zinaendelea.

0 Comments:
Post a Comment