Mgombea Udiwani kata ya Makiba Bi Joyce Martin Lutha (Wa pili kutoka kulia) akiwa na viongozi wengine wa Chadema kuhitimisha mkutano wa kampeni wa chama hicho Jana. |
Taarifa iliyotufikia usiku huu ni kwamba watu wanaodhaniwa ni wafuasi wa chama cha mapinduzi CCM wamevamia nyumbani kwa Mgombea wa Udiwani kata ya Makiba Joyce Martin Lutha wakiwa na Jeshi la Polisi katika jimbo la Arumeru Magharibi.
Tukio hili linajiri wakati ambapo zimebaki saa chache kuelekea uchaguzi wa Marudio wa Udiwani kwenye kata 43 nchini unaotarajiwa kufanyika hapo Kesho mapema jumapili ya 26/November.
Taarifa hiyo ya dharura imedai mawakala watano wa chama hicho pamoja na pikipiki zao wamekamatwa usiku huu haijabainika haraka ni idadi ya Pikipiki ngapi zimekamatwa.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure ameliambia Habari Tanzania kuwa Kama uongozi wa chama hicho wamepokea taarifa hizo kwa huzuni na kwamba "Hii ni hujuma Mbaya sana kwa Democrasia na mfumo wa Vyama vingi Vya Siasa nchin." Alisema Mungure
Jitihada za kuipata Jeshi la Polisi usiku huu zimekwama Baada ya kupiga simu nyingi za OCD wa Meru ambapo simu yake haikupatikana huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha naye hakupatikana kwenye simu yake.

0 Comments:
Post a Comment