CHADEMA Wafunga Mikutano ya kampeni Rasmi..

Katibu wa Chadema mkoa wa Manyara nazidi kubaki kwenye headlines ambapo Leo amehutimisha mkutano wa kampeni kwenye kata ya Makiba katika kijiji cha Valeska kwenye jinbo la Arumeru Mashariki.

Mungure Akishirikiana na Mbunge wa  Sumanjiro Mh. James Ole Millya Walifunga mkutano wa mwisho wa kampeni za Udiwani kata ya Makiba ambapo Jana ulifanyika kwenye viunga vya kijiji cha Valeska.

Katika Hotuba yake Millya amesema chadema ni chama makini na wala hakitatukana kama vyama vingine vinavyotumia majukwaa ya siasa kututukana amesema Chadema ni chama makini hivyo kesho 26/November Wananchi wapige kura za ndiyo kwa Mgombea Udiwani kata Ya Makiba Chadema Joyce Martin Lutha.

Uchaguzi Mdogo wa marudio nchini unatarajiwa kukamilika hapo kesho kwa wapiga kura kuamua wenyewe kupitia sanduku la kura kumchagua nani wa chama gani.

0 Comments:

Post a Comment