FULL VIDEO: Boss wa AVE Ltd alivyokabidhi Million 15 kwa Vikundi vya Kijasiriamali Levolosi Arusha

Grace Macha Mkurugenzi wa Kampuni ya Arusha Vicoba Empowerment Ltd amekabidhi Miamala ya Kibenki kwa Vikundi Vitatu ambavyo ni Levolosi Native Association , Watano Group , na Baraka Group.
Afisa Mtendaji mtaa wa Levolosi Cecilia Ngowi akimkabidhi Muamala wa Kuwekewa Fedha Tsh Million 5 benki Mwakilishi wa kikundi cha Levolosi Native Association.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa niaba ya Halmashauri ya jiji la Arusha Arusha vicoba empowerment ltd wanekuwa wakiiwakilisha Serikali kwa kuvipatia Vikundi vya kijasiriamali vilivyopitishwa ili kupata 10% ya mikopo kwa ajili ya Wanawake na Vijana.

Tazama video Hapa Grace Macha akikabidhi Fedha Hizo.
Aidha Baada ya Kukabidhiwa fedha hizo Vikundi hivyo vikapata Fursa ya kueleza namna wanavyofaidika na mikopo hiyo.

Video ya VOA TV News hapa chini inamuonesha Mama Huyu Ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi cha Baraka Group kwenye Kata ya Levolosi ambayo ni miongoni mwa Vikundi Vitatu vilivyopewa Mikopo ya Tsh. Million 5 kwa kila kikundi.

0 Comments:

Post a Comment