Mkuu wa Wilaya ya Arusha DC Gabriel Daqaro amewataka vijana kujikita katika kujiunga na vikundi vya kijasiriamali ili kujikwamua kimaendeleo.
Akizungumza na wawakulishi wa vikundi hivyo Leo katika ukumbi wa Shule ya Arusha School Mkuu Wilaya amesema vijana wamekuwa wazembe katika kujiingiza kwenye fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuchukua mikopo.
Akifanya ufunguzi wa Mafunzo kwa vikundi vya kijasiriamali Mali jijini Arusha DC Daqarro pia amekabidhi Hundi ya Tsh Millioni 605. Kwa ajili ya Vikundi vya Wanawake , Vijana na makundi ya walemavu.
Aidha DC Daqarro amesema inasikitisha mno Wanawake kuwa na muamko Mkubwa katika kuchangamkia fursa za maendeleo huku wimbi la vijana likiangamia na matendo maovu yasiyofaa . Hivyo amewataka vijana kuamka nakuachana na starehe za kuhonga ili wajikwamue kiuchumi.
Katika Mgawanyo wa fedha hizo za mikopo Leo DC Daqarro amekabidhi Fedha Hindi ya Tsh. Millioni 505 kwa ajili ya kina mama (Wanawake) , Na Millioni 100 kwa ajili ya vijana.
Katika hafla hiyo Vikundi 121 zote kwenye Halmashauri ya jiji la Arusha vinaendelea kupatiwa mafunzo ili kuhakikisha fedha wanazopewa wanatumia ipasavyo na kurejesha kwa wakati.


0 Comments:
Post a Comment