DC Daqarro akabidhi Hundi ya Tsh Millioni 605 kwa Vikundi vya Wanawake , Vijana na Walemavu

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro (wa pili Kutoka Kushoto) Akikabidhi Hundi ya Tsh. 505 kwa Vikundi vya kijasiriamali Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha DC Gabriel Daqarro Leo amekabidhi Hundi ya Tsh Millioni 505 kwa Vikundi vya wanawake (Kina Mama) na Millioni 100 kwa Vikundi vya Vijana.

DC Gabriel Daqarro Amesema Hayo ndiyo matarajio na matunda ya serikali ya awamu ya tano ambayo hufanya kazi yake kwa vitendo chini ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

DC Daqarro alialikwa kufanya ufunguzi wa Semina ya mafunzo kwa Vikundi vya kijasiriamali vya vijana na wanawake (Kina mama) ufunguzi uliofanyika Leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Arusha Schools.

Awali akizungunza kwenye Hotuba yake DC Daqarro amesisitiza Kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa zinazokuwepo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi na kuleta maendeleo kwanu vijana ni nguvu ya Taifa.

Katika hatua Nyingine DC Daqarro amewataka Kina Mama kuwashawishi vijana wao kujiunga kwenye Vikundi vya kijasiriamali ili kuepukana na vitendo viovu ambavyo hurudisha Maendeleo nyuma.

Aidha katika kuhitimisha Hotuba yake DC Daqarro akatoa rai kwa vijana ambao wamebahatika kupata mkopo huo kuutumia ipasavyo na kuepukana na vishawishi ambavyo vitaleta ukwamishi wa kutokufikia malengo tarajiwa ikiwa ni pamoja na kutojiingiza kwenye starehe mbalimbali ya Ulevi , Uasherati ambayo huishia kupata magonjwa kama ukimwi na kukwamisha ndoto.

Mafunzo hayo kwa Vikundi vya kijasiriamali yanaendelea huku agenda kubwa ikiwa kuwafunza wana Vikundi jinsi ya kutumia mikopo hiyo Kwa malengo waliyotarajia na kurejesha mikopo kwa wakati ili kurahisisha Vikundi vingine kupata Mikopo.

0 Comments:

Post a Comment