SABA WAACHIWA HURU KESI YA WAFANYAKAZI EXIM BANK ARUSHA


MAHAKAMA ya hakimu mkazi Arusha imewaachia huru washitakiwa saba  waliokuwa wafanyakazi wa benki ya Exim Arusha huku ikiwaweka hatiani washitakiwa wengine sita.

Washitakiwa hao alikuwa wanakabiliwa na mashitaka 318 utakatishaji fedha haramu,kughushi nyaraka,kuharibu nyaraka na wizi wa zaidi Shilingi Biloni Saba katika benki hiyo.


Uamuzi huo umetolewa leo na Kaimu hakimu mkazi mfawidhi, Desder Kamugisha aliyesikiliza shauri hilo la jinai namba 309/2013.

Washitakiwa walioachiwa huru ni Bimal Gondalia, Neema Kinabo, Livingston Julius, Evance Kashebo, Tuntufye Agrey, Josephat Neki na Gervas Lubuva.

Waliowekwa hatiani ni Lilian Mgeye, Daudi Mosha, Dorothy Tigana, Genes  Massawe,Christopher Lyimo na Deusdedit Chacha.

Aidha katika kesi hiyo jamhuri walikuwa na vielelezo 20 ikiwemo benki slip za malipo ya wateja wa kampuni mbalimbali za kitalii,zilizokuwa zikilipwa katika benki hiyo kwa ajili ya wageni wa nje waliokuwa wakienda katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA),vocha na nyaraka nyingine ziliwasilishwa.

Kwa sasa hakimu anaandika adhabu nitawahabarisha zaidi

0 Comments:

Post a Comment