UPDATESzaUCHAGUZI: Lowassa Atikisa Arumeru Mashariki Azuru Mikutano Miwili ndani saa chache na kupewa zawadi nono , MUNGURE Atia neno.

Lowassa Akikabidhiwa Zawadi ya Shuka la Kimasai na wazee wa kimila kama ishara ya Heshima. Hafla iliyofanyika katika mkutano wa kampeni Kata ya Ngabobo Arumeru Mashariki Leo.
Wananchi wa kata Ngabobo waliojitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano wa Kampeni wa uchaguzi Mdogo Arumeru Mashariki. Mkutano uliohudhuriwa na Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na mjumbe wa baraza kuu la CHADEMA Taifa Edward Lowassa amehudhuria mkutano wa kampeni cha uchaguzi wa marudio uliofanyika katika kata ya Ngabobo Arumeru Mashariki Mkoa wa Arusha.

Lowassa ameambatana na Viongozi wa wa CHADEMA  Mkoa wa Arusha akiwemo Katibu wa chama hicho Mkoa wa Arusha Mh.  Elias Mungure , Katibu mwenezi Wilaya ya Arusha Mh. Paulo Tingatinga.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elias Mungure

Awali Lowassa alipokelewa na wazee wa kimila wa Kata ya Ngabobo katika kikao Maalum cha ndani kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa mkutano.

Aidha Lowassa amemnadi Mgombea Udiwani Kata ya Gambobo Bw. Emanuel Fanuel na kuwa ifikapo November 26 wamchague Mgombea huyo kwa wingi huku akiahidi kutembelea kara hiyo endapo wakazi hao watampigia kura Mgombea huyo.

Wazee wa kata ya Ngabobo walionesha tofauti katika mkutano huo wa Kampeni kwa lumzawadia mzee Lowassa Shuka la Kimasai,Mbunge Joshua nasari, na Mgombea Udiwani Emanuel Fanuel kwa kile walichodai ni kuwaamini viongozi hao.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari akikabidhiwa zawadi ya Shuka na wazee wa kimila kata ya Ngabobo Arumeru Mashariki Leo.

Aidha Katibu wa chama hicho Mkoa wa Arusha Mh Elias Mungure amesema chama hicho hakitumii bunduki kushinda ".....CHADEMA hatumiu bunduki kupigana ..CHADEMA hatutumii polisi kushinda tunafuata Sheria na Katibu kushinda..."

LOWASSA AHUDHURIA MKUTANO WA KAMPENI LEGURUKI.
Maelfu kwa maelfu ya wakazi wa kata ya Leguruki walifurika kuwasikiliza Viongozi wa CHADEMA pamoja na Mgombea Udiwani Rabriel Mbise 

Katika Hatua nyingine Waziri huyo Mkuu wa Zamani wa Tanzania alizuru kata ya Leguruki kwa ajili ya kumnadi Mgombea Udiwani katika kata hiyo Bw. Rabiel Mbise anayewania nafasi hiyo kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Diwani wa kata hiyo miezi kadhaa iliyopita.

Viongozi wa CHADEMA Mkoa wakiongozwa na Katibu Mh. Elias Mungure wa Mkoa Arusha walihutubu na kuzungumzia mengi ikiwa ni pamoja na sababu ya wananchi kupiga kura katika uchaguzi huo wa matudio.

Pamoja na shughuli kubwa ya kumnadi Mgombea Udiwani katika kata hiyo Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari alihutubu akizungumzia jinsi walivyompigania Diwani aliyefikia hatua ya kunivua nyadifa aliyopewa na wananchi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.
Miradi ya maji , afya , Elimu nako havikusahaulika katika mkutano huo wa kampeni.

Aidha Mzee Lowassa akaeleza sababu ya kutokuitisha maandamano baada ya madai ya kura zake kuibiwa baada ya kufanyika uchaguzi wa October 25 ikiwa ni pamoja kuhofia umwagaji damu. Lowassa amesema "ukiupata urais kwa damu utauacha kwa damu.." 

Katika mikutano yote Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elias Mungure amekuwa akisisitiza neno HAKI katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika hapo November 26. "CHADEMA hatutumii Bunduki , CHADEMA hatutumii Polisi kushinda tunatumia sheria na Katibu ya nchi..." 

Mungure aliongeza kuwa haki itendeke katika uchaguzi huo na kwamba mithili yao ya kuwapeleka mahakamani watakaokwenda kinyume na taratibu za uchaguzi upo tayarj hivyo alionya kwa msisitizo suala la uwizi wa kura.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI LEO KWENYE KAMPENI ZA CHADEMA KATA YA LEGURUKI ARUMERU MASHARIKI.


0 Comments:

Post a Comment