![]() |
| Picha ya Mkutano wa kampeni za CHADEMA leo kwenye kata ya Ambureni Arumeru Mashariki. |
Karibu maeneo yote ambako CHADEMA imefanya mkutano kumekuwa na Mwitikio na hamu kubwa ya wananchi kutaka kufika kwenye mikutano ya kampeni ya chama hicho Hivyo hali hiyo kupelekea Chadema kueonekana kuwa na wafuasi wengi nchini.
Wengine husema chama hicho kipo kwenye damu za watu kwa sababu ya Sera zake lakini hakuna mwenye kujua ukweli huu ya hilo ila pengine huenda likawa kweli.
Habaritanzaniagracemacha.com pamoja na VOA TV News tumezunguka karibu kwenye mikutano yote ya vyama vya Siasa vinavyowania kitu cha madiwani kwenye kata 43 nchini kwahyo tumejionea wenyewe hali ya Siasa kwenye majukwaa na sasa tunalingoja kwenye sanduku la kura.
![]() |
| Mkutano wa chama hicho kata ya Makiba jimbo la Aruneru Mashariki. |
Kwa jinsi hali ilivyo na kama itaenda hivyo hivyo basi CHADEMA kushinda ni Asubuhi kwenye maeneo yote ya uchaguzi wa marudio. Ila kama ni Wananchi wanakwenda kkandhuria tu basi hali hii itakuwa tofauti wataalam husema visevesa .
Jimbo la Arumeru Mashariki lenye kata nyingi za uchaguzi Mdogo wa Marudio imeonekana kuwa ngome haswa ya upinzani tofauti na ilivyofikiriwa hapo awali kutokana na Wimbi kubwa la kujiuzulu madiwani lilianzia huko.
Haya ni maoni na wala hayalengi kupendelea upande wowote na pia hayana Sehemu yoyote kwenye taratibu zote za uchaguzi unaondelea nchini...
Tathmini zinaonesha CHADEMA kushika nafasi ya kwanza CCM ikishikilia nafasi ya pili na Maeneo Mengine ushindani ni Mkubwa baina ya vyama hivi vitatu vya ACT-Wazalendo , CCM na CHADEMA.


0 Comments:
Post a Comment