LATEST NEWS: CHADEMA wafanya mkutano wa Kihistoria Ambureni, Arusha Lowassa atoa Sababu ya Kushindwa Urais Uchaguzi Mkuu 2015

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Mh.Elias Mungure akihutubu kwenye mkutano wa kampeni kwenye kata ya Ambureni Leo.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeendelea na kampeni zake mkoani Arusha ambapo Leo kampeni za chama hicho zimefanyika katika kata ya Ambureni jimbo la uchaguzi la Arumeru Mashariki.
Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya akihutubu kwenye mkutano wa Kampeni Leo Ambureni Arusha 
Mkutano wa Chadema uliouhudhuriwa na Maelfu ya Wananchi umeshuhudia ujio wa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amvaye pia ni mnumbe wa baraza kuu la Chama hicho Taifa , Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya , Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro na  mwenyeji wao Joshua Nasari Mbunge wa Arumeru Mashariki pamoja na viongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure.

Katika mkutano wa kata ya Ambureni Leo viongozi mbalimbali kitaifa walipata fursa ya kusema na umati Mkubwa wa watu uliohudhuria katika mkutano huo wa kampeni.

Awali Katibu wa Mkoa CHADEMA Elias Mungure alifafanua lengo na dhumuni la kusanyiko hilo kuwa ni kuwaeleza wananchi kuwa chama hicho kina watu makini na Mara baada ya hapo akamkaribisha stejini Mstahiki Meya wa jiji La Arusha Kalisti Lazaro.
Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro
Kalisti Lazaro amesema kimsingi madiwani wanaojiuzulu wamewadhalilisha madiwani wengine nakuwaomba wana Ambureni msamaha kwa kitendo hicho alichodai cha aibu. Meya ameawataka Wananchi wa Ambureni kumchagua Diwani wa Chadema anayegombea kiti hicho kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika November 26 mwaka huu.
Katika hatua nyingine Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya akawataka wananchi wa kata Ambureni wasifanye makosa katika uchaguzi huo huku akisisitiza kuwa wasikatishwe tama.

LOWASSA ASEMA SABABU YA KUSHINDWA URAIS 2015

Aidha Lowassa katika hotuba yake kwa wakazi wa Ambureni ilijikita katika sakata la katiba mpya ambapo alieleza kuwa kilichomfanya asishinde kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 ni ubovu wa katiba na kusisitiza kuwa kunahitajika Katiba mpya ili kuweka uwiano sawa kwenye shughuli za kidemokrasia nchini.

PICHA NA MATUKIO KUTOKA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI ZA CHADEMA KATA YA AMBURENI ARUMERU MASHARIKI ARUSHA.



Katibu mwenezi wa CHADEMA Arumeru Mashariki  Paulo Tinga Tinga

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elias Mungure


0 Comments:

Post a Comment