XCLUSIVE: Johnson Mahuma amwagiwa sifa Uchaguzi wa Marudio Arusha

Bw. Johnson Mahuma
Johnson Mahuma Mgombea Udiwani uchaguzi wa Marudio Kata ya Muriet jijini Arusha amepata sifa nyingi sana kutoka kwa Wananchi na viongozi wa chama chake cha ACT-Wazalendo hivyo akionekana na uwezo mkumbwa wa kutatua Kero zinazowakabili wakazi wa Muriet.

Vyama vya CCM ,CHADEMA na ACT-Wazalendo Vimesimamisha wagombea Muriet huku Johnson Mahuma kupitia ACT-Wazalendo Akionekana kuwa na ushawishi Mkubwa kwa Wananchi na wakazi wa Muriet. 
Juma hili Jicho letu la uchaguzi halikusita kupita Muriet kukuarifu japo kinachoendelea Katika harakati za kampeni za vyama vinavyoshindania kiti hicho cha Udiwani Kumrithi Diwani kwa tiketi ya CHADEMA Credo Fukwe aliyejiuzulu kwa madai ya kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli 

Baada ya kuzinduliwa rasmi leo Kumefanyika Kampeni ya ACT-Wazalendo Maeneo ya Baa Mpya Kwa mrombo sokoni Katika Kata ya Muriet Wananchi walifurika Kusikiliza sera za Mgombea Johnson Mahuma na Mara baada ya Kampeni kumalizika VOA TV News Ikampata Katibu wa Jimbo la Arusha mjini ACT-Wazalendo Daudi Mkwizu ambaye amemwagia sifa Mgombea wao.. Tazama video hapa chini..
Aidha Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa hakusita kumnadi na kumsifia Mgombea Huyo Bw. Johnson Mahuma.

Kampeni za Chama hicho zinaendelea maeneo mbalimbali nchini ambapo kunafanyika uchaguzi wa Marudio. 

Hata hivyo Mh. Mahuma anatarajiwa kwenda kumnadi Mgombea wa Chama hicho katika Kata ya Moita wilayani Monduli hapo Novemba 8 Mwaka huu.

Endelea kubaki na VOA TV News #Updates #Xclusives & Habaritanzaniagracemacha.com na usipitwe na chochote..

0 Comments:

Post a Comment